logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Karim Benzema atangaza kustaafu soka la kimataifa

Benzema alikosa Kombe la Dunia nchini Qatar kutokana na jeraha la paja.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo20 December 2022 - 03:41

Muhtasari


  • •Alicheza mechi 97 na anashika nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji mabao wa muda wote wa Ufaransa akiwa na mabao 37.

Karim Benzema ametangaza kustaafu soka la kimataifa, siku moja baada ya Ufaransa kushindwa na Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2022.

Benzema alikosa michuano hiyo nchini Qatar kutokana na jeraha la paja na hakuweza kuchezea Ufaransa tena.

Alicheza mechi 97 na anashika nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji mabao wa muda wote wa Ufaransa akiwa na mabao 37.

"Nilifanya juhudi na makosa niliyochukua ili kuwa hapa nilipo na ninajivunia hilo!" Benzema alituma ujumbe huo katika mitandao yake ya kijamii. "Nimeandika hadithi yangu na yetu inaisha."

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ufaransa alishinda tuzo ya Ballon d'Or - tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka huu - kwa mara ya kwanza.

Benzema alifunga mabao 44 katika michezo 46 alipoisaidia Real kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga msimu wa 2021-22.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved