Mashabiki 20K wasaini ombi la kutaka Alvarez wa Man-City kumuacha mpenzi wake

Ombi hilo ambalo limesainiwa na watu wengi linajiri wakati mpenzi huyo alikataa Alvarez asipige picha na mashabiki.

Muhtasari

• Sasa inatarajiwa kuonwa kama mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia atatekeleza ombi hilo ama atazidi kugandiana na mchumba wake kwa mapenzi yasiyojua kufa.

Mshambuliaji wa Man City atakwa kuacha mpenzi wake
Mshambuliaji wa Man City atakwa kuacha mpenzi wake
Image: Instagram

Wafuasi wa mchezo wa soka wamejumuika mtandaoni kutia saini ombi la kumtaka mshambuliaji wa timu ya Manchester City na timu ya taifa ya Argentina kinda Julian Alvarez kumbwaga mpenzi wake wa muda mrefu kwa jina Emelia Ferrero.

Kulingana na jarida la Mirror, ombi hilo ambalo lilianzishwa na mtumizi mmoja wa mitandao ya kijamii tayari limetiwa saini na watu zaidi la elfu 20.

Lakini je, ni kwa nini watu wanataka kinda huyo wa miaka 22 kuachana na mpenzi wake? Jarida hilo lilitoa sababu,

“Shabiki mmoja aliyekasirika alikasirishwa sana na kukataa kwa mshawishi wa YouTube Emelia Ferrero kuruhusu kikundi cha watu wanaovutiwa kupiga picha na mpenzi wake wakati wa sherehe za kijanja za Argentina hivi kwamba walikata rufaa wakimwomba Alvarez amalize uhusiano wao wa miaka mine.”

Sasa inatarajiwa kuonwa kama mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia atatekeleza ombi hilo ama atazidi kugandiana na mchumba wake kwa mapenzi yasiyojua kufa.

Alvarez alipata umaarufu baada ya timu ya City kumsaini kutoka kwa timu ya River Plate kwa dau la pauni milioni 14 tu.

Alifana sana katika kombe la dunia ambapo alikuwa kama mshambuliaji wa kutegemewa na alifunga mabao manne kuisaidia Argentina kunyakua ubingwa wa dunia kwa mara ya tatu katika historia ya taifa hilo.

Alvarez amefunga mabao saba na kutoa asisti mbili katika mechi 20 baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Guardiola majira ya joto. Baada ya kufumania nyavu mara nne wakati Argentina iliposhiriki kombe la dunia Qatar, thamani yake imepanda sana - lakini Guardiola ameweka wazi kuwa mchezaji huyo aliyepewa jina la utani ‘Spiderman’ ana mustakabali mkubwa na mabingwa hao.