Ronaldo azuiliwa kushiriki mechi 2 za Al Nassr kufuatia tukio la kupasua simu ya shabiki

Mchezaji huyo alifungiwa mechi mbili Novemba lakini hakushiriki na United hadi kuondoka kwake.

Muhtasari

• Ronaldo kwa hasira aliangusha na kupasua simu ya shabiki wa Everton aliyetaka kupiga picha naye baada ya Man U kupoteza ugani Goodson Park.

Al Nassr yazuiliwa kumchezesha Ronaldo kufuatia kumshambulia shabiki wa Everton.
Al Nassr yazuiliwa kumchezesha Ronaldo kufuatia kumshambulia shabiki wa Everton.
Image: Instagram

Baada ya timu ya AL Nassr kumsaini nyota wa Ureno Christiano Ronaldo, mchezaji huyo alikuwa anatarajiwa kushiriki mchezo wake wa kwanza kama mchezaji wa Al Nassr hii leo Alhamisi dhidi ya Al Ta’ee.

Lakini hilo halitowezekana kutokana na marufuku aliyopewa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kufuatia kuivunja simu ya shabiki wa Everton aliyetaka kupiga picha naye.

Kulingana na jarida la Daily Mail, mchezaji huyo anayejiita ‘wa kipekee’ ambaye aliondoka Manchester United kwa dharau, bado anastahili kuadhibiwa kwa kosa na ameambiwa amezuiwa kuichezea Al Nassr kwa mechi mbili zaidi.

Alipatikana na hatia ya tabia isiyofaa na ya jeuri baada ya kuvunja simu ya shabiki wa Everton kutoka mkononi mwake baada ya United kupoteza mechi katika uwanja wa Goodison Park Aprili mwaka jana.

Aliupiga mkono wa Jacob Harding huku akishuka chini kwenye mtaro na kuharibu simu ya kijana huyo.

Wakati uchunguzi ukiendelea mwezi uliopita, iliripotiwa kuwa Ronaldo angekubali mashtaka ya mwenendo usiofaa kutoka kwa FA, lakini alikuwa amedhamiria kupambana na tishio la kufungiwa.

FA walimfungia mechi mbili mwezi Novemba baada ya kitendo hicho lakini hakuwahi kuichezea United tena mpaka kuelekea kombe la dunia na baadae kuondoka timuni humo.

Marufuku hiyo inaendelea kwa klabu yake inayofuata na kuizuia Al Nassr kumchezesha mshambuliaji wake mpya hadi itakapocheza mechi mbili za kimashindano ambazo angekuwa tayari kucheza.