Christiano Ronaldo kupigwa marufuku kafuatia sakata la usajili haramu wa Juventus

Klabu ya Juventus inachunguzwa kwa kufanya usajili wa mikataba ya kinyemela kati ya mwaka 2019 na 2020.

Muhtasari

• Ronaldo alijiunga na Juventus mwaka 2018 akitoka Real Madrid.

• Sasa imebainika kuwa Juventus iliwashawishi sajili zao mpya kukubali kukatwa mishahara ili kujiunga nao, hivyo kusababisha hasara kwa mizania.

• Ikiwa wachezaji hoa watapatikana na hatia, huenda wakapigwa marufuku ya kujihusisha na masuala ya soka, haijalishi bado wapo Juve au waliondoka.

Ronaldo adokolewa macho na marufuku kwa mkataba wa kinyemela Juventus
Ronaldo adokolewa macho na marufuku kwa mkataba wa kinyemela Juventus
Image: Mirror

Wiki jana shirikisho la soka nchini Italia lilitangaza kuinyanganya timu ya Juventus pointi 15 kwa tuhuma za kufanya usajili wa wachezaji kati ya mwaka 2019 hadi 2021 kwa njia za kinyemela kinyume na sheria za shirikisho hilo.

Sasa imeibuka kuwa kando na timu hiyo kuadhibiwa kwa kunyanganywa pointi, bado kuna adhabu nyingine zaidi zinakuja pindi uchunguzi utakapokamilika.

Wachezaji wa sasa na wa zamani kipindi hicho ambao walikuwa katika timu hiyo huenda wakajipata katika upande mbaya wa sheria kwa kufungiwa baada ya kubainika kuwa huenda walikubali kuingia katika mkataba na timu hiyo kwa njia za kinyemela.

Mwandishi wa habari wa Kiitaliano Paolo Ziliani anaamini kwamba ikiwa wachezaji hao watapatikana kwa uongo kukubali mishahara ya chini, basi watawajibika kwa adhabu ya kufungiwa kwa siku 30, bila kujali kama bado wako klabuni au la.

Wachezaji hao wanachunguzwa kwa kughushi kuyumbishwa kwa mishahara yao ili kufanya hasara kutoweka kwenye mizania. Juu ya orodha hii ni Cristiano Ronaldo ambaye aliichezea Juventus kwa miaka mitatu kabla ya kwenda Manchester United. Sasa yuko Saudi Arabia na Al-Nassr.

Kando na wachezaji, pia imebainika kuwa watu wengine ambao huenda wakatiwa hatiani ni aliyekuwa kocha wa Juventus kipindi hicho Maurizio Sarri, msimamizi wa usajili katika timu ya Tottenham Hotspurs Fabio Paratici miongoni mwa wengine.

Orodha hiyo pia inajumuisha watu kama wachezaji Rodrigo Bentancur, Federico Bernardeschi,  Leonardo Bonucci, Giorgio Chiellini, Juan Cuadrado, Gianluigi Buffon, Danilo, Matthijs de Ligt,  Mattia De Sciglio, Merih Demiral, Douglas Costa, Paulo Dybala, Gonzalo Higuain, Sami Khedira, Alex Sandro, Blaise Matuidi, Miralem Pjanic, Adrien Rabiot, Aaron Ramsey, Cristiano Ronaldo, Daniele Rugani, Wojciech Szczęsny na kocha Maurizio Sarri.