Man U yaibuka timu bora na yenye thamani kubwa katika ligi kuu ya Premia

Timu hiyo ilishika usukani mbele ya watani wa jadi Arsenal, Liverpool, Mancity na Chelsea.

Muhtasari

• United kwa sasa ndio timu pekee kutoka Uongereza iliyosalia katika mashindano ya mataji 4 tofuati.

• United inafukuzia ubingwa wa Premia, ligi ya Uropa, kombe la FA na ngao ya Carabao.

Manchester United
Manchester United
Image: Manchester

Kwa mara nyingine tena, timu ya soka ya Manchester United imeibuka kidedea kama timu yenye thamani kubwa zaidi katika ligi kuu ya Premia nchini Uingereza.

Katika orodha ambayo imetolewa hivi karibuni, Manchester United wametajwa kama timu yenye thamani kubwa zaidi na kuwabwaga wapinzani wao wa karibu kama Mabingwa watetezi wa taji la Premia Manchester City, watani wa jadi Arsenal na wababe Liverpool.

Hili linakuja licha ya timu hiyo kukaa bila kushinda ligi ya Premia kwa miaka 10 sasa tangu kufanya hivo mara ya mwisho wakiwa na kocha mstaafu Sir Alex Ferguson mwaka 2013.

United wanazidi kufurahia mwenendo mzuri uwanjani msimu huu chini ya Erik ten Hag, ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu wa joto kuchukua nafasi ya Ralf Rangnick.

Ndio timu ya pekee kutoka Uingereza ambayo imesalia katika mashindano ya mataji zaidi ya matatu yakiwemo ubingwa wa ligi ya Uropa, ligi kuu ya Premia, taji la FA na ngao ya Carabao mtawalia.

Kulingana na jarida la Sportico, United ina thamani ya pauni bilioni 4.8 huku Liverpool wakiwanyemelea kwa ukaribu kwa thamani ya pauni bilioni 3.8.

Orodha hiyo inaendelea kwa timu ya Manchester City yenye thamani ya pauni bilioni 3.5, Arsenal wanafunga nne bora kwa utajiri wa pauni bilioni 2.9.

Chelsea wanaikaribia Arsenal katika nafasi ya tano na utajiri wa pauni bilioni 2.8 huku Tottnham Hotspurs Tottenham pauni bilioni 2.6, West Ham wakiwa na thamani ya pauni milioni 539, Everton pauni milioni 486, Leicester pauni milioni 442, na Newcastle wakihitimisha kumi bora kwa utajiri wa pauni milioni 357.