Mchezaji wa zamani wa Chelsea ni miongoni mwa waliokwama kwenye vifusi vya jengo Uturuki

Mtetemeko wa ardhi ulikumba taifa hilo usiku wa Jumapili na kuporomosha majumba mengi ambapo mamia ya watu wamenaswa.

Muhtasari

• Juhudi za uokoaji zingali zinaendelea.

Christian Atsu, aliyekuwa mchezaji wa Chelsea.
Christian Atsu, aliyekuwa mchezaji wa Chelsea.
Image: Twitter

Usiku wa kuamkia Jumatatu dunia iliamkia taarifa mbaya kuhusu zilizala ya kishindo iliyotokea nchini Uturuki.

Mtetemeko huo wa ardhi uliporomosha majumba mengi chini na kuwanasa ndani mamia ya watu na shughuli za uokoaji zinaendelea kulingana na majarida ya nchini humo.

Taarifa za hivi punde zinadai kuwa aliyekuwa winga wa Chelsea na Newcastle Christian Atsu ni miongoni mwa watu ambao wamenaswa kwenye vifusi hivyo.

Jarida la Kituruki Star linadai kuwa operesheni ya kumtafuta na kumwokoa nyota huyo inaendelea baada ya kukutwa na tetemeko la ardhi la 7.8 siku ya Jumatatu.

Atsu, 31, alijiunga na klabu ya Super Lig Hatayspor akitokea Al-Raed ya Saudia msimu uliopita.

Na wanachama kadhaa wa timu yake mpya walilazimika kuokolewa na wataalamu nyumbani kwao baada ya tetemeko la ardhi kupiga saa kumi asubuhi kwa saa za huko.

Lakini inadaiwa kwamba  Atsu na mkurugenzi wa michezo wa Hatayspor Taner Savut wanasalia kupotea chini ya vifusi kwenye nyumba zao.

Tetemeko la ardhi lilipiga sana huko Kahramanmaras, ambapo kuna makazi ya Hatayspor.

Wachezaji wawili na wafanyakazi wa kiufundi "walitolewa kwenye vifusi" katika shughuli kadhaa za uokoaji. Na juhudi bado zinaendelea kuwatafuta waliowahi kucheza kwa mkopo Everton Atsu na Savut haraka iwezekanavyo, The Sun waliripoti.

Sio mwanasoka pekee aliyekosekana, huku mlinda lango wa Yeni Malatyaspor Ahmet Eyup pia akinaswa.

Zaidi ya watu 1,000 wanaaminika kufariki katika tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki mwendo wa saa nne asubuhi Jumatatu.