Mchezaji wa soka afariki akiwa uwanjani mechi ikiendelea

Beki huyo wa miaka 21 alifariki baada ya kukimbizwa hospitalini alipougua wakati wa mechi ya divisheni ya kwanza.

Muhtasari

• Taarifa Zaidi kuhusu kifo cha mchezaji huyo hazijatolewa bado.

Moustapha Sylla, mcezaji wa Ivory Coast
Moustapha Sylla, mcezaji wa Ivory Coast
Image: Twitter

Mchezaji wa soka nchini Ivory Coast katika ligi ya divisheni ya kwanza alifariki wikendi iliyopita wakati wa mechi.

Kulingana na taarifa za AFP, mchezaji hyo kwa jina Moustapha Sylla mweney umri wa miaka 21 alipatwa na matatizo ya kiafya wakati mechi ingali bado inaendelea na alikimbizwa hospitalini lakini akasemekana kufariki dunia.

"Beki wetu Moustapha Sylla alifariki jioni ya leo kufuatia kuugua uwanjani wakati wa mechi ya RCA vs Sol FC," ilisema taarifa ya klabu Racing d'Abidjan.

"Wakati wa kuhamishwa kwake hospitalini, Moustapha alifariki. Alifika klabuni Septemba mwaka jana na alikuwa na umri wa miaka 21 pekee," rais wa klabu Logossina Cisse alithibitisha kwa AFP.

Racing d'Abidjan walikuwa mabingwa wa kitaifa mwaka wa 2020 na kwa sasa wako nafasi ya saba kwenye michuano hiyo.

Taarifa Zaidi kuhusu kifo cha mchezaji huyo hazijatolewa bado.