Mashetani Wekundu wabanduliwa nje Europa

United walikuwa chini ya kiwango chao na walizidiwa nguvu karibu kila dakika.

Muhtasari

•United walifanya makosa mawili mabaya katika safu yao ya ulinzi -yaliyowagharimu kwa kuchapwa 3-0.

•Katika mechi ya kwanza Old Trafford wakiwa mbele kwa mbwembwe kwa mabao 2-0, yakarudi na kwenda sare ya 2-2.

Image: BBC

Manchester United imefungasha virago michuano ya Ulaya baada ya kuchapwa na Sevilla katika mzunguko wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Europa.

United walikuwa chini ya kiwango chao – walizidiwa karibu kila idara na mbaya zaidi walifanya makosa mawili mabaya katika safu yao ya ulinzi -yaliyowagharimu kwa kuchapwa 3-0.

Katika mechi ya kwanza Old Trafford wakiwa mbele kwa mbwembwe kwa mabao 2-0, yakarudi na kwenda sare ya 2-2.

Kikosi hicho cha Erik ten Hag ni kama kimeruhusu mabao matano ndani ya dakika 90 - mabao mawili ya dakika za mwisho huko Manchester na matatu Jana Hispania.

Sevilla iko nafasi ya 13 kwenye Ligi Hispania (La Liga) na wametumia muda mwingi wa msimu mbaya kupambana kukwepa kushuka daraja, lakini walionekana kuimarika tena chini ya Jose Luis Mendilliba, meneja wao wa tatu wa kudumu msimu huu.

Sevilla sasa itakutana na Juventus iliyoiondosha Sporting CP kwa jumla ya mabao 2-1, kufuatia sare ya 1-1 jana. Mchezo wa awali Juve ilishinda 1-0.