Hongera! Mkenya, Kelvin Kiptum ashinda mbio za London Marathon

Kiptum aliweka rekodi ya pili kwa kasi katika mbio za marathoni.

Muhtasari

Kiptum alitwaa ushindi baada ya kukimbia kwa muda wa saa 2:01:25 na kuweka rekodi ya pili kwa kasi katika mbio za marathoni.

•Geofrey Kamworor alikuwa mshindi wa pili kwa mara ya pili mfululizo mjini London.

Kelvin Kiptum
Image: HISANI

Bingwa wa Valencia Marathon mwaka wa 2022, Kelvin Kiptum ndiye bingwa wa mwaka huu wa London Marathon.

Kiptum alitwaa ushindi baada ya kukimbia kwa muda wa saa 2:01:25 na kuweka rekodi ya pili kwa kasi katika mbio za marathoni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliweka rekodi mpya ya mbio za London juu ya iliyowekwa na Eliud Kipchoge mwaka wa 2019 kwa zaidi ya dakika.

Alikuwa sekunde 16 tu nje ya rekodi ya dunia ya Kipchoge ambayo ni 2:01:09

Mwezi Desemba mwaka jana, Kiptum aliweka muda wa tatu kwa kasi zaidi wa 2:01:53 katika marathon yake ya kwanza.

Geofrey Kamworor ambaye ameshinda mbio za marathon za New York mara mbili alikuwa mshindi wa pili kwa mara ya pili mfululizo mjini London.

Muingereza Mo Farah alimaliza wa tisa katika kile anachosema kuwa itakuwa marathon yake ya mwisho.