Wachezaji 6 na kocha wapewa kadi nyekundu kufuatia mzozo uwanjani

Wachezaji sita walitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za ziada, watatu kutoka pande zote

Muhtasari

• Kulingana na viwango vya Superclasico, mechi hiyo ilikuwa mojawapo ya mchuano mkali zaidi kuwahi kutokea katika ulingo wa soka barani America Kusini

•Refa aliwatoa nje wachezaji watatu kutoka kila upande pamoja na kocha wa Boca, Jorge Almiron.

Wachezaji wa timu ya River plate wapinzana na wale wa Boca juniors.
Wachezaji wa timu ya River plate wapinzana na wale wa Boca juniors.

Wachezaji 6 walionyeshwa kadi ya nyekundu wakati wa mechi baina ya River plate na Boca Juniors kwenye ligi kuu ya Argentina. Saba hao walitimuliwa uwanjani katika dakika za nyongeza baada ya mzozo mkubwa wa dakika 15 uliofuatia bao la penalti la River Plate katika dakika ya 90 iliyowapatia ushindi.

Kulingana na viwango vya Superclasico, mechi hiyo ilikuwa mojawapo ya mchuano mkali zaidi kuwahi kutokea katika ulingo wa soka barani America Kusini. Mechi hiyo ilishuhudia taharuki kubwa katika dakika za mwisho.

Wachezaji sita walitolewa kwa kadi nyekundu katika muda ulioongezwa, watatu kutoka kwa pande zote, wakati mzozo mkubwa ulipozuka muda mfupi baada ya penalti ya River Plate kuchelewa na kuwafanya kuwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Boca.

Wasimamizi na maafisa wa kutuliza ghasia walilazimika kuingilia kati kusaidia kutawanya timu hizo na hatimaye mambo yalipopoa, refa aliwatoa nje wachezaji watatu kutoka kila upande pamoja na kocha wa Boca, Jorge Almiron.

River plate ambayo inasimamiwa na kocha Martin Demichelis, ilishikilia ushindi kutokana na mkwaju wa penalti wa Miguel Borja kwenye uwanja wa Estadio Monumental.

Borja alionyesha ujasiri wake katika hali ngumu zaidi, na kumpeleka  kipa wa zamani wa Manchester United, Sergio Romero upande wa kushoto huku akipiga mkwaju wake upande wa kulia katika dakika ya 93 na rabsha ilizuka  kutokana na majibu ya Romero.

Ushindi huo uliwasaidia River plate kuimarisha uongozi wao katika ligi hio ya Argentina.