SOKA KIMATAIFA

Mwamuzi katika fainali ligi ya mabingwa 2023 avumbuliwa

Aliamua katika nusu fainali ya City na Real Madrid mkondo wa pili

Muhtasari

• Szymon Marciniak mwenye uraia wa Poland ndiye atakuwa refa wa kati katika fainali  ligi ya mabingwa kati ya Manchester City na Inter Milan itakayoandaliwa Istanbul nchini Uturuki Juni 10.

• Mpolandi huyo msimu huu ameamua  katika shindano hilo mara nane, hasa katika nusu fainali  kati ya Man City na Real Madrid mkondo wa pili.

• Hii itakuwa fainali yake ya kwanza tangu alipohudumu kama mwamuzi wa nne mwaka wa 2018.

Szymon Marciniak mwenye uraia wa Poland,imebainika kuwa ndiye atakuwa mwamuzi wa kati katika ngarabe  ya fainali  ya ligi ya mabingwa kati ya Manchester City na Inter Milan itakayoandaliwa Istanbul nchini Uturuki Juni 10.

Mpolandi huyo msimu huu ameamua  katika shindano hilo mara nane, hasa katika nusu fainali  kati ya Man City na Real Madrid mkondo wa pili. Hii itakuwa fainali yake ya kwanza tangu alipohudumu kama mwamuzi wa nne mwaka wa 2018.

Marciniak 42, pia alikuwa mwamuzi katika shindano la kombe la ulimwengu kati ya Ufaransa na Ajentina Disemba 2022. Refa huyo atasaidiwa na Pawel Sololnicki na Tomasz Listkiewicz,huku  mwamuzi wa nne akiwa Istvan Kovacs na afisaa wa VAR Tomsz Kwiatkowski.

Mwaka wa 2023,Szymon Marciniak alitatajwa kama mwamuzi bora, na shirikisho la soka kimataifa.

Hii itakuwa fainali ya pili kwa City  baada ya kupoteza mikononi mwa Chelsea 2021 na kubanduliwa katika hatua ya nusu fainali na vigogo wa Uhispania Real Madrid 2022.

kwa upande wake Klabu ya Inter Milan, wamelinyakua taji hilo mara tatu,ikiwa ni katika mwaka wa 1964,1965 na 2020.