Mason Mount aondoka uwanjani akilia katika kile kinaonekana ni kwaheri kwa Chelsea

Kinda huyo hakuwa fiti kucheza lakini baada ya mechi kukamilika na mashabiki kuondoka, alibaki uwanjani ambapo alionekana akizunguka machozi yakimlenga lenga.

Muhtasari

• Mkataba wa Mount unamalizika mwishoni mwa msimu ujao na Chelsea wako tayari kumuuza.

• Arsenal na Newcastle pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.

 

Mason Mount aondoka uwanjani akilengwa na machozi.
Mason Mount aondoka uwanjani akilengwa na machozi.
Image: Getty IMAGES

Mason Mount alionekana mwenye hisia kali alipoondoka Stamford Bridge baada ya kile kinachoweza kuwa kuaga kwake Chelsea.

Kiungo huyo hakuwa fiti kucheza katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle, lakini alijiunga na wachezaji wengine wa timu hiyo walipofanya mzunguko wa jadi wa kushukuru baada ya mechi.

Mount alirejea uwanjani mara tu mashabiki walipoondoka na kuonekana mwenye hisia kali aliposhiriki kukumbatiana na mfanyikazi wa chumba cha kubadilishia nguo cha Chelsea.

Manchester United na Liverpool wanawania kumsajili Mount, ambaye anaonekana uwezekano mkubwa wa kuihama klabu yake ya utotoni msimu huu wa joto.

Kocha mkuu anayekuja Mauricio Pochettino amedokeza kuwa anataka kusalia Mount lakini bado hana ushawishi wowote juu ya mustakabali wake huku kukiwa na mvutano wa kandarasi na Chelsea.

Mkataba wa Mount unamalizika mwishoni mwa msimu ujao na Chelsea wako tayari kumuuza ili kuhakikisha wanapokea ada ya uhamisho na hawahatarishi kumpoteza bure msimu ujao wa joto.

Arsenal na Newcastle pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Cesar Azpilicueta, Pierre-Emerick Aubameyang, Ruben Loftus-Cheek, Trevoh Chalobah, Edouard Mendy, Christian Pulisic na Mateo Kovacic walikuwa miongoni mwa wachezaji wa Chelsea ambao pia walishiriki katika kipindi cha shukrani na wangeweza kuichezea klabu hiyo mechi yao ya mwisho.