Mbappe asema haendi Real Madrid

Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Barcelona na Uhispania Luis Enrique anatarajiwa kuwa meneja ajaye wa Paris St-Germain.

Muhtasari
  • Ni Karim Benzema na Robert Lewandowski pekee waliopita jumla ya mabao 16 ya Joselu kwenye La Liga msimu uliopita.
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Image: Maktaba

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, anasema atasalia Paris St-Germain msimu ujao na kuamua mustakabali wake 2024 mkataba wake utakapokamilika. (Telefoot, kupitia 90min)

Mbappe alifunga mara 29 kwenye Ligue 1 msimu uliopita na kuisaidia PSG kushinda taji la 11 la ligi kuu.

Sport (kwa Kihispania) inaripoti kwamba Real Madrid wamejiondoa katika harakati bza kumsajili Mbappe na watatangaza kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Joselu, 33, kutoka Espanyol wiki hii.

Ni Karim Benzema na Robert Lewandowski pekee waliopita jumla ya mabao 16 ya Joselu kwenye La Liga msimu uliopita.

Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Barcelona na Uhispania Luis Enrique anatarajiwa kuwa meneja ajaye wa Paris St-Germain. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Luis Enrique amekuwa hana kazi tangu ajiuzulu nafasi yake na Uhispania baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora kwenye Kombe la Dunia la 2022.

Alihusishwa na Tottenham na Chelsea kabla ya kuwateua Ange Postecoglou na Mauricio Pochettino mtawalia.