Beki wa Chelsea Ben Chilwell aomboleze kifo cha baba yake

Hata hivyo, Chlwell alifajikia katika kile alisema kuwa japo atamkosa sana babake, lakini ataishi na furaha kwamba babake aliishi kuona ndoto ya mwanawe kuichezea timu ya taifa ya Uingereza ikitimia.

Muhtasari

• Dadake Ben, Alex Chilwell, alithibitisha habari hiyo siku ya Jumatatu na kukiri kuwa ulikuwa mwaka "mgumu" kwa familia huku risala za rambi rambi zikimimika kwenye mitandao ya kijamii.

Ben Chilwell akiwa na baba yake Wayne Chilwell.
Ben Chilwell akiwa na baba yake Wayne Chilwell.
Image: INSTAGRAM/ CHILWELL

Beki wa Chelsea, Ben Chilwell yuko katika majonzi kufuatia kifo cha babake, Wayne Chilwell baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika ujumbe aliyochapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, Chilwell alimuomboleza baba yake kama nguzo muhimu kwa mafanikio yake katika soka.

"Sababu niko hapa nilipo. Baba mwenye upendo zaidi, ambaye kila mara aliweka kila mtu mbele yake na kufanya kila mtu atabasamu na kucheka. Nina furaha sana tulipata kuishi ndoto yangu pamoja, na haswa ukiniona nikicheza kwa mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya  Uingereza.” Chilwell alichapisha ujumbe wa kuhuzunisha.

Dadake Ben, Alex Chilwell, alithibitisha habari hiyo siku ya Jumatatu na kukiri kuwa ulikuwa mwaka "mgumu" kwa familia huku risala za rambi rambi zikimimika kwenye mitandao ya kijamii.

“Nakupenda milele baba, mwaka mgumu zaidi lakini hukuacha kutabasamu. Ninafuraha sana kwa muda tulioshiriki nawe. Ninahisi nikama nimepotea sana bila wewe. Niangalie n unichunge ukiwa huko juu.   Nakupenda  Nakupenda.” Aliandika dada yake Chilwell.

Mchezaji huyo muhimu wa timu ya Chelsea alikuwa sehemu ya kikosi cha wanablues kilichoishinda Manchester City na kushinda Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge.

Chilwell aidha alikosa kushiriki michuano ya kombe la dunia baada ya kupata jeraha la goti alilolipata mwezi Novemba siku chache tu kabla ya shindano hilo kuanza.

Miongoni mwa wachezaji wenzake waliojitokeza na kutuma risala za rambirambi naye ni pamoja na Mason Mount, beki mwenzake Reece James na wengine.