Mwanasoka Benjamin Mendy alikiri kulala na wanawake 10,000 - Mlalamishi

Mwanasoka huyo alikanusha mashtaka yote mawili dhidi yake.

Muhtasari

• Mlalamishi aliambia mahakama kuwa mchezaji huyo aliwahi kumwambia kuwa amewahi kulala na zaidi wanawake 10,000..

• Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 28 anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, katika jumba lake la kifahari.

Benjamin Mendy, 28, anakanusha makosa manane ya ubakaji, shtaka moja la kujaribu kubaka na moja la unyanyasaji wa kingono.
Benjamin Mendy, 28, anakanusha makosa manane ya ubakaji, shtaka moja la kujaribu kubaka na moja la unyanyasaji wa kingono.
Image: BBC

Mwanamke anayedaiwa kubakwa na beki wa Manchester City, Benjamin Mendy aliambia mahakama kuwa mchezaji huyo aliwahi kumwambia kuwa amewahi kulala na zaidi wanawake 10,000.

Kulingana na ushuhuda wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 mbele ya mahakama, Mendy alimnyanyasa kimapenzi kisha akamwambia "ni sawa, nimefanya mapenzi na wanawake 10,000."

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 28 anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, katika jumba lake la kifahari la pauni milioni 4 katika mtaa wa Mottram St Andrew, Cheshire, mnamo Oktoba 2020.

Pia anatuhumiwa kwa jaribio la kumbaka mwanamke mwingine, mwenye umri wa miaka 29 wakati huo, ambaye alisema pia alimshambulia nyumbani kwake miaka miwili kabla ya tukio hilo.

Mwanasoka huyo alikanusha mashtaka yote mawili dhidi yake.

Bw Aina (kiongozi wa mashataka) alisema kuwa mchezaji huyo alikutana kwa mara ya kwanza na mwanamke A, mwanafunzi chini Uingereza, akiwa katika klabu moja jijini Barcelona mwishoni mwa 2017 na akawa na urafiki wa karibu na mmoja wa marafiki zake.

Waliendelea kuwasiliana na mwaka mmoja baadaye alipanga kwenda kumtembelea rafiki wa mshtakiwa kwenye nyumba ya mwanasoka huyo, ambapo walikaa baada ya wote kwenda na wasichana wengine ili kupumzika usiku huo.

Asubuhi iliyofuata, alipokuwa akioga katika chumba chake cha kulala, Mendy alionekana akiwa amevalia chupi tu na "kusisimka kingono", mahakama ilisikiza.

Beki huyo ndipo anadaiwa kumshika mwanamke huyo na kujaribu kumbaka kitandani alipokuwa akijitahidi kujiweka huru kutoka kwa mikono ya Mendy.

Miaka miwili baadaye, mwanamke B alikuwa ametoka na marafiki zake kwenye baa moja huko Alderley Edge, Cheshire, karibu na nyumbani kwa Mendy, walipoalikwa kurudi nyumbani kwa mwanasoka huyo.

Mwanamke huyo anadai mshtakiwa alimnyang'anya simu yake, iliyokuwa na picha za "kisiri", kisha kumpeleka kwenye chumba chake cha kulala, huku akimuomba arudishiwe simu yake.

Bw Aina alisema Mendy alimwambia "Nataka tu kukutazama" na kumwambia avue nguo zake.

Mwanamke B alitii, nakusalia tu na chupi, kisha Mendy akaitupa simu yake kitandani.

Alipokuwa akienda kuichukua, mwanasoka huyo anadaiwa kumshika kwa nyuma na kumbaka licha ya kumwambia hataki kushiriki ngono.

Bw Aina aliambia jaji: "Katika hatua hii Mendy alirudi nyuma na kusema 'una uoga sana'.

"Bwana Mendy alisema, 'Ni sawa. Nimefanya mapenzi na wanawake 10,000'." alisema kuiongozi wa mashtaka.

Mchezaji kandanda huyo aliwaambia polisi kuwa katika tukio zote mbili vitendo vyote vya kingono vilikuwa ya makubaliano na walalamishi na kukanusha madai yoyote.