Mfahamu 'Neymar wa Senegal' anayetarajiwa kuisisimua Chelsea

Mwishoni mwa msimu uliopita, aliwekwa kama mshambuliaji wa Villarreal na alionesha umahiri wake.

Muhtasari

•Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapenda kutamba na mpira na alikuwa mchezaji mwenye 10% bora Ulaya msimu uliopita kwa kutamba na mpira mbele.

•Kwa kuhamahama, harakati zake za mara kwa mara zitamfanya kuwa mwiba kwa walinzi wa Premier League ambao walizoea mashambulizi ya Chelsea msimu uliopita.

Image: BBC

Akiwa karibia kuhamia klabu ya Bournemouth mwezi Januari kutokana na jraha lililomkatisha tamaa, Nicolas Jackson sasa anajikuta kama mchezaji wa Chelsea.

Kwa hivyo "Neymar wa Senegal" ataleta nini kwa Mauricio Pochettino?

Kama jina lake la utani linavyopendekeza, akicheza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapenda kutamba na mpira na alikuwa mchezaji mwenye 10% bora Ulaya msimu uliopita kwa kutamba na mpira mbele

Ana werevu mwingi akimiliki mpira na haoni aibu kuutumia – Ni Vinicius Junior wa Real Madrid pekee ndiye aliyechangia mabao mengi baada ya kupiga chenga katika ligi kuu tano za Ulaya kuliko Jackson 2022-23.

Alipogunduliwa kwa mara ya kwanza, nafasi yake aliyoipenda zaidi ilikuwa kwenye bawa la kushoto, akikata ndani hadi mguu wake wa kulia alioupenda zaidi.

Hata hivyo, mwishoni mwa msimu uliopita, aliwekwa kama mshambuliaji wa Villarreal na alionesha umahiri wake, akimaliza kampeni akiwa na mabao tisa katika mechi nane.

Je ni Jibu la matatizo ya Chelsea ya kufunga mabao? Ingawa si mshambuliaji wa kati wa kawaida anayefanana na nyota wa Manchester City Erling Haaland, Jackson anaweza kufanya mashambulizi kwenye safu ya ushambuliaji na ni hatari anapopewa nafasi.

Alipiga wastani wa mashuti mawili pekee kwenye goli kwa kila mechi msimu uliopita, lakini alifunga moja kati ya matatu. Hilo lilimweka katika 2% ya juu kwa washambuliaji wote wa Uropa mnamo 2022-23.

Kwa kuhamahama, harakati zake za mara kwa mara zitamfanya kuwa mwiba kwa walinzi wa Premier League ambao walizoea mashambulizi ya Chelsea msimu uliopita.

Yeye ni mrefu, lakini uwezo wake wa angani unahitaji kazi, kwa hivyo wafuasi wowote wa Blues wanaotarajia kuwa na umbo la Didier Drogba watakatishwa tamaa.

Hata hivyo, kutokana na viungo vyake , ujana , umri wake na rekodi ya Pochettino katika kuwang'oa wachezaji chipukizi, ushahidi unaonyesha kuwa Chelsea wamesajili mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa.