Man United wanatarajia kukamilisha dili la kumnunua kipa wa Inter Milan, Andre Onana

Mkataba wa De Gea huko Old Trafford ulimalizika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Muhtasari

•Mkufunzi wa United Erik ten Hag ana nia ya kusuluhisha wasiwasi kuhusu hali ya walinda mlango Old Trafford.

•Hag alimfundisha Onana katika Ajax na Mholanzi huyo anaamini kuwa mchezaji huyo yuko katika kiwango anachohitaji .

Image: BBC

Manchester United wana matumaini ya kukamilisha dili la kumnunua kipa wa Inter Milan Andre Onana.

Mkufunzi wa United Erik ten Hag ana nia ya kusuluhisha wasiwasi kuhusu hali ya walinda mlango Old Trafford huku kukiwa na sintofahamu juu ya mustakabali wa David de Gea.

Mkataba wa De Gea huko Old Trafford ulimalizika mwishoni mwa mwezi uliopita bila makubaliano kuhusu ofa iliyopitiwa tena aliyopewa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uhispania.

Onana, 27, alicheza pasi nane katika mechi 24 kwenye Serie A msimu uliopita.

Mcameroon huyo pia alipeana pasi nane bila mabao katika mechi 13 za Ligi ya Mabingwa msimu uliopita - nyingi zaidi ya golikipa yeyote katika shindano hilo.

Hag alimfundisha Onana katika klabu ya zamani ya Ajax na Mholanzi huyo anaamini kuwa mchezaji huyo yuko katika kiwango anachohitaji na atazoea maisha ya Ligi Kuu kwa urahisi.

Kinyume chake, Ten Hag haamini kwamba uwezo wa De Gea akiwa na mpira miguuni mwake uko kwenye kiwango kinachohitajika.