• Klabu hiyo ilianza mchakato mrefu wa kuboresha uwanja wao mwishoni mwa msimu uliopita.
• Barca itacheza mechi za nyumbani za msimu ujao kwenye Uwanja wa Olympic mjini Montjuic.
Timu ya Barcelona italazimika kutafuta uwanja mbadala msimu kesho baada ya uwanja wao wa nyumbani Nou Camp ukianza kubomolewa tayari kwa ukarabati.
Katika video moja ambayo imepakiwa na jarida la Mundo Deportivo kwenye ukurasa wao wa Twitter, inaoehsa mashine nzito zikibomoa uwanja huo wenye historia ndefu ya klabu hiyo miamba wa Uhispania.
Uwanja huo mashuhuri unapata mabadiliko kidogo katika msimu wa joto na mchakato huo ulianza siku ya Jumatatu wakati mashine zilipoanza kubomoa.
Klabu hiyo ilianza mchakato mrefu wa kuboresha uwanja wao mwishoni mwa msimu uliopita. Barca itacheza mechi za nyumbani za msimu ujao kwenye Uwanja wa Olympic mjini Montjuic.
Hawatarejea kwenye uwanja wao hadi mwishoni mwa 2024, kwani Camp Nou itafunguliwa tena kwa asilimia 70 yenye uwezo wa kuezekea paa na paneli za jua.
Kikosi cha wakubwa kilirejea katika kituo cha mazoezi cha klabu hiyo kwa ajili ya mitihani ya afya siku ya Jumatatu huku wakianza maandalizi yao ya msimu ujao.