Samuel Eto'o akabiliwa na wito wa kujiuzulu kama mkuu wa FA wa Cameroon

Samuel Eto'o, ambaye ameongoza FA ya Cameroon tangu Desemba 2021, amekosolewa kwa baadhi ya maamuzi yake ya hivi majuzi.

Muhtasari

•Wiki iliyopita, Chama cha Vilabu vya Wachezaji wa Ridhaa nchini Cameroon (ACFAC) kilipiga kura 11-1 kuunga mkono kumtaka Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne ajiuzulu.

Samuel Eto'o, ambaye ameongoza FA ya Cameroon tangu Desemba 2021, amekosolewa kwa baadhi ya maamuzi yake ya hivi majuzi.
Samuel Eto'o, ambaye ameongoza FA ya Cameroon tangu Desemba 2021, amekosolewa kwa baadhi ya maamuzi yake ya hivi majuzi.
Image: BBC

Kundi linalowakilisha vilabu vya wachezaji soka wa ridhaa nchini Cameroon limemtaka mchezaji maarufu wa zamani Samuel Eto'o kujiuzulu wadhifa wake kama rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo, kwa sababu ya "ukiukwaji mkubwa" katika shirika hilo.

Wiki iliyopita, Chama cha Vilabu vya Wachezaji wa Ridhaa nchini Cameroon (ACFAC) kilipiga kura 11-1 kuunga mkono kumtaka Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne ajiuzulu.

Kilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42, ambaye alichezea vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya, anapaswa kujiuzulu "ikiwa bado anapenda soka ya Cameroon, kama ambavyo amekuwa akidai kila mara".

ACFAC ilitoa wito kwa waziri wa michezo wa Cameroon kuingilia kati, na kutaja uwezekano wa kumtaka rais wa Fifa Gianni Infantino kufanya hivyo.

Miongoni mwa yale yanayolalamikiwa na, ACFAC n pamoja na uamuzi wa kubadilisha mamlaka ya rais wa Fecafoot kutoka miaka minne hadi saba ulikuwa kinyume na sheria na kinyume cha sheria.

Pia ilionyesha ukosefu wa uchapishaji wa sheria mpya zilizopitishwa Agosti iliyopita.