Harambee Stars imepangwa katika Kundi 'F' la kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026

Stars itamenyana na Shelisheli, Burundi, Gambia, Gabon na Côte d’Ivoire.

Muhtasari

• Mechi ya kwanza ya kufuzu kwa mikondo miwili itachezwa kati ya Novemba 13 na Novemba 21.

• Washindi wa kila kundi watafuzu moja kwa moja kwa mashindano hayo.

Harambee Stars
Image: FACEBOOK

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imepangwa katika Kundi 'F' la kufuzu kwa Kombe la Dunia la Fifa 2026 dhidi ya Ushelisheli, Burundi, Gambia, Gabon na Côte d'Ivoire.

Stars walikuwa kwenye Chungu cha 3 cha droo iliyochezewa Abidjan, Cote d'Ivoire, Alhamisi, Julai 13.

Mechi ya kwanza ya kufuzu kwa mikondo miwili itachezwa kati ya Novemba 13 na Novemba 21.

Washindi wa kila kundi watafuzu moja kwa moja kwa mashindano hayo.

Zaidi ya hayo, washindi wanne bora kutoka kwa makundi watafuzu kwa michuano ya Caf ya mchujo, ambayo mshindi wake atajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya 2026.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu ya taifa kurejea katika michuano ya Caf na Fifa baada ya kupigwa marufuku ya mwaka mzima na shirikisho hilo.