Mlindalango wa PSG na mkewe washambuliwa na kuporwa Paris

Kengele ililia na wafanyakazi wa hoteli waliowaondoa wawili hao na kuwapeleka hospitalini.

Muhtasari
  • Wanandoa hao walilengwa na watu kadhaa na kufungwa kwenye nyumba yao katika wilaya ya nane katikati mwa mji mkuu,

Mlindalango wa Italia na Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma na mwenzake wameshambuliwa na kuibiwa nyumbani kwao mjini Paris.

Wanandoa hao walilengwa na watu kadhaa na kufungwa kwenye nyumba yao katika wilaya ya nane katikati mwa mji mkuu, vyanzo vya polisi vimeambia vyombo vya habari vya Ufaransa.

Wanaripotiwa kutorokea kwenye hoteli iliyo karibu.

Kengele ililia na wafanyakazi wa hoteli waliowaondoa wawili hao na kuwapeleka hospitalini.

"Uchunguzi umefunguliwa kuhusu mashitaka ya wizi wa kutumia silaha katika genge lililopangwa na ghasia zilizokithiri kufuatia matukio yaliyotokea usiku wa kuamkia leo mahali pa Bw Donnarumma," msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris aliambia BBC.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa kwenye tovuti ya habari ya Actu17 zinasema washambuliaji waliondoka na vito, saa na bidhaa za ngozi za kifahari zenye thamani ya takriban €500,000 (£430,000).

Mwanasoka huyo alijeruhiwa kidogo huku mpenzi wake, mwanamitindo Alessia Elefante, akiripotiwa kuwa hajajeruhiwa, duru zililiambia Shirika la habari la AFP.

Katika taarifa, wakala wake alisema Gianluigi Donnarumma, 24, na mpenzi wake "wameshtushwa na kile kilichotokea lakini wanaendelea vizuri chini ya hali mbaya. Wote wanasaidia polisi kwa maswali yao".

Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema kitengo maalum cha polisi cha BRB cha Ufaransa kinacholenga wizi wa kutumia silaha na wizi kimeanza uchunguzi.

Article share tools