Saudi Pro League: Cristiano Ronaldo anavyoongoza mapinduzi katika soka la Asia

Al-Nassr wameshuhudia kuongezeka kwa mauzo ya shati, hasa yenye jina la Ronaldo

Muhtasari

•Tangu Cristiano Ronaldo ajiunge na Al-Nassrr, nchi hiyo imekuwa katika uangalizi wa kimataifa wa soka na Jezi ya njano ya klabu inazidi kufahamika Ulaya na kwingineko.

•Nguvu mpya ya kifedha ya nchi katika soka, hata hivyo, imeiweka katika kiwango tofauti kabisa uwanjani.

Image: BBC

Huenda timu za Ligi Kuu ya Uingereza zinatatizika kukubaliana na vilabu vya Saudi Arabia vinavyowahamisha baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa lakini mashabiki wa Riyadh, Jeddah na miji mingine mikubwa ya Mashariki ya Kati na Asia pia wanalazimika kuzoea hali mpya ya soka.

Tangu Cristiano Ronaldo ajiunge na Al-Nassr - moja ya vilabu vya 'Big Four' pamoja na wapinzani wa Riyadh Al-Hilal na wababe wa Jeddah Al-Ittihad na Al-Ahli – tangu mwezi Desemba, nchi hiyo imekuwa katika uangalizi wa kimataifa wa soka na Jezi ya njano ya klabu inazidi kufahamika Ulaya na kwingineko.

"Kutazama rangi ya manjano au 'The Yellow' ikienea duniani kote kunaniridhisha na kunifurahisha sana lakini pia ninahisi mwaminifu kwa ligi ya nchini," shabiki wa Nassr

Ligi ya Saudia itatawala barani Asia?

Huku timu ya taifa ikishiriki katika michuano sita ya Kombe la Dunia na vile vile kushinda makombe matatu ya bara la Asia huku vilabu vikiwa vimeshinda Ligi ya Mabingwa wa Asiamara sita, Saudi Arabia imekuwa ikitamba katika kanda na bara.

Nguvu mpya ya kifedha ya nchi katika soka, hata hivyo, imeiweka katika kiwango tofauti kabisa uwanjani.

'Cristiano alifanya kile kinachochukua miaka kufanya'

Al-Nassr wameshuhudia kuongezeka kwa mauzo ya shati, hasa yenye jina la Ronaldo
Al-Nassr wameshuhudia kuongezeka kwa mauzo ya shati, hasa yenye jina la Ronaldo
Image: BBC

Wachezaji nyota sio tu kwamba huleta ubora zaidi lakini pia wameundwa ili kusababisha mashabiki zaidi, mikataba ya matangazo, udhamini, mauzo ya bidhaa na uwekezaji.

Lengo la Saudi Arabia ni kwamba ligi hiyo iwe katika 10 bora zaidi duniani kwa kupata mapato ifikapo 2030.

Tayari, kuna ishara chanya za kibiashara.

Al-Nassr watacheza na Benfica siku ya Alhamisi kisha watamenyana na Paris St-Germain na Inter Milan nchini Japan baadaye mwezi huu.

Klabu hiyo pia imetia saini mkataba wa jezi na kampuni ya Nike, huku afisa mmoja akiambia BBC kwamba miamba hiyo ya mavazi ya Marekani inaweza kusaidia kuhakikisha shati za njano zinazovaliwa kote ulimwenguni ni rasmi.

Mnamo Novemba, kulikuwa na ziara 10,000 kwa ukurasa wa bidhaa wa tovuti ya klabu.Mnamo Januari - mwezi ambao Ronaldo alisaini - idadi hiyo iliongezeka hadi 300,000.

"Tumeona mashati mengi ya Al-Nassr tangu msimu uliopita na inaongezeka sana," anasema Mohammed.

"Cristiano alifanya mara moja kile kinachochukua kampeni za uuzaji na nyara miaka mingi kufanya.

"Tulicheza dhidi ya Celta [Jumatatu] na mashabiki wengi walikuwa pale wakiwa wamevalia shati ya Nassr yenye jina la Cristiano nyuma na nembo ya Nassr mbele.

"Yote ni juu ya kuongeza kiwango, ni uboreshaji kama huo."