BBC walazimika kuomba radhi kwa kuuliza mchezaji wa Morocco swali la ushoga

"Nchini Morocco, ni kinyume cha sheria kuwa na uhusiano wa mashoga. Je, una wachezaji mashoga kwenye kikosi chako na maisha yao yakoje huko Morocco?" - mwanahabari wa BBC aiuliza.

Muhtasari

• Ni mara ya kwanza kwa nchi ya Kiarabu kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake.

•  Nchini Morocco, mahusiano ya jinsia moja kwa wanaume na wanawake ni kinyume cha sheria, huku ushoga ukihukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela.

BBC AIMETOA TAMKO LA RADHI KWA SWALI YA KISHOGA KWA NAHODHA WA MOROCCO.
BBC AIMETOA TAMKO LA RADHI KWA SWALI YA KISHOGA KWA NAHODHA WA MOROCCO.
Image: TWITTER, BBC,

Shirika la habari la BBC limeomba msamaha kufuatia maswali yao "yasiyofaa" kwa nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Morocco katika Kombe la Dunia la Wanawake.

Hali hii ilijitokeza wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kabla ya mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Ujerumani.

Ripota kutoka BBC News World Service alimuuliza Ghizlane Chebbak swali ambalo linaweza kuathiri usalama wa mwenzake nyumbani, akiuliza: "Nchini Morocco, ni kinyume cha sheria kuwa na uhusiano wa mashoga. Je, una wachezaji mashoga kwenye kikosi chako na maisha yao yakoje huko Morocco?"

Msimamizi wa mkutano wa FIFA aliingilia kati: "Samahani, hili ni swali la kisiasa sana, kwa hivyo tutazingatia tu maswali yanayohusiana na mpira wa miguu."

Mwanahabari huyo, bila kutubu, alijibu: "Hapana, sio ya kisiasa, ni ya watu, haina uhusiano wowote na siasa. Tafadhali mwache ajibu swali.”

Mkutano huo wa wanahabari ulihitimishwa kwa swali moja tu kutoka kwa vyombo vya habari.

Ni mara ya kwanza kwa nchi ya Kiarabu kuwahi kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake. Nchini Morocco, mahusiano ya jinsia moja kwa wanaume na wanawake ni kinyume cha sheria, huku ushoga ukihukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela.

Kulingana na Human Rights Watch, Morocco inaadhibu tabia ya watu wa jinsia moja kwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela na faini ambayo inakiuka kati ya dirham 120-1,000 (£25 - £212).

BBC sasa wameona inafaa kuomba msamaha kwa safu ya maswali. Taarifa ya BBC ilisema: "Tunatambua kuwa swali hilo halikuwa sahihi. Hatukuwa na nia ya kusababisha madhara yoyote au dhiki.”

The Atlas Lionesses, kama timu ya wanawake ya Morocco inavyojulikana, ilipoteza kwa mabao 6-0 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wao wa ufunguzi. Sasa wanaelekea katika mchezo wao wa pili wa kundi Julai 30 dhidi ya Korea Kusini.