Arsenal imezundua sanamu ya Arsène Wenger nje ya Uwanja wa Emirates

Sanamu hiyo imetengenezwa kwa shaba, yenye uzani wa takriban nusu tani, na ina urefu wa mita 3.5, na inasherehekea Arsène Wenger kunyanyua taji la Ligi Kuu - ambalo alishinda mnamo 1998, 2002 na 2004.

Muhtasari

• Aliisaidia klabu hiyo kutoshindwa katika ligi wakati wa kutwaa ubingwa wa 2004 na timu inayojulikana kama "The Invincibles."

• Arsenal pia walitumia misimu 20 mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa chini ya Wenger, ikiwa ni pamoja na kufika fainali ya 2006.

Arsenal wamempa heshima yake Arsenal Wenger
SANAMU Arsenal wamempa heshima yake Arsenal Wenger
Image: ARSENAL

Klabu ya mpira wa soka ya Arsenal nchini ingereza wamezindua sanamu ya kocha wao wa muda mrefu Arsène Wenger nje ya Uwanja wa Emirates siku ya Ijumaa, wakiadhimisha mchango wa ajabu wa Arsène kwa klabu hiyo ya London Kaskazini.

“Wakati wake kama meneja wetu, Arsène alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu na saba ya Kombe la FA, na hivyo kutufikisha kwenye msimu wa kihistoria wa ligi bila kushindwa katika 2003/04,” sehemku ya taarifa kwenye tovuti ya Arsenal ilisoma.

Sanamu ya Arsène iliundwa na mchongaji aliyeshinda tuzo Jim Guy, akifanya kazi na mkurugenzi wa usimamizi wa bidhaa Ian Landor katika MDM.

Muda wa utayarishaji ulikuwa takriban mwaka mmoja na sanamu ilitolewa na timu ya Waanzilishi ya Simon Allan na Adam Paddon kutoka Sculpture Castings, ripoti hiyo ilizidi kusoma.

Sanamu hiyo imetengenezwa kwa shaba, yenye uzani wa takriban nusu tani, na ina urefu wa mita 3.5, na inasherehekea Arsène Wenger kunyanyua taji la Ligi Kuu - ambalo alishinda mnamo 1998, 2002 na 2004.

Wenger alihudumu kama mmoja wa makocha waliokaa kweney klabu moja kwa muda mrefu Zaidi katika historia ya ligi kuu ya Uingereza EPL, ikiwa ni kutoka mwaka 1996 hadi 2018.

Mfaransa huyo aliweza kuchezesha mechi 1,235 akiwa na Arsenal na aliisaidia klabu hiyo kutoshindwa katika ligi wakati wa kutwaa ubingwa wa 2004 na timu inayojulikana kama "The Invincibles."

 

Arsenal pia walitumia misimu 20 mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa chini ya Wenger, ikiwa ni pamoja na kufika fainali ya 2006, ambapo walichapwa 2-1 na Barcelona.

Kwa mujibu wa jarida la ESPN, Wenger atakuwa mgeni wa heshima wa klabu hiyo kwa mechi ya Kombe la Emirates dhidi ya Monaco siku ya Jumatano na anatarajiwa kuzuru sanamu hiyo siku zijazo.

Sanamu yake inaungana na wengine watano -- wakiwa na Tony Adams, Dennis Bergkamp, ​​Herbert Chapman, Ken Friar na Thierry Henry -- kwenye jukwaa kuzunguka Uwanja wa Emirates.

"Alinichagua kuwa mmoja wa wachezaji wake na kunichagua kuwa nahodha wa klabu na hilo ni jambo ambalo sitalisahau," meneja wa sasa wa Arsenal Mikel Arteta alisema.