Man U wabanwa koo,wapoteza mechi tatu mfululizo michuano ya kirafiki

Mashetani Wekundu mambo yamewaendea mrama, wamefungwa mabao manane kwa mechi tatu!

Muhtasari

•Manchester United watakuwa na kibarua Agosti 14 watakapokuwa wakikabiliana na Wolves katika mechi ya kwanza msimu mpya 2023/2024.

Rashford akanusha United kukata tamaa.
Rashford akanusha United kukata tamaa.
Image: Twitter

Miamba wa soka katika ligi kuu nchini Uingereza Manchester United wameweza kupoteza katika mechi za kirafiki mara tatu mfululizo.

Michuani hiyo ambayo iliandaliwa Ujapani, klabu hiyo ya Ten Hag imejipata katika kibarua kigumu katika mechi zilizotangulia, kwani licha ya kufanya usajili wa hali ya juu kwa wachezaji waliojawa na tajriba.

Washindi hao wa ligi ya Premier mara 13, wamekuwa wakijiandaa kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa 2023/2024, ambapo wamekuwa mbioni kusakamana na mahasimu wake katika ligi hiyo pamoja na mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi Manchester City.

Mambo ya vijana hao wa United yalianza kutumbukia nyongo wakati ambapo meneja ErikTen Hag alitanguliza vijana wenye umri mdogo kutoka akademi ya klabu hiyo kukabiliana na Wrexham, ambapo walipata kibano cha 1_3.

Kando na hayo, klabu hiyo pia ilipata kichapo cha mabao mawili bila jawabu na vigogo wa soka katika ligi ya Uhispania Real Madrid, ambapo mashabiki wa klabu hiyo waliingilia na kumkashifu mlinda lango Adre Onana kwa kufanya kosa lililochangia kushindwa kwao.

Hayo hayatoshi kwani mapema Jumatatu, Mashetani Wekundu waliraukia kichapo cha mabao 3_2 dhidi ya Borussia Dortimund, licha ya mchezaji wa kiungo wa Diogo Dalot kutangulia kufunga katika dakika ya 23.

Baadhi ya wachezaji klabu hiyo imeweza kusajili katika msimu huu wa joto ni pamoja na Adre Onana kutoka Inter Milan, aliyesajiliwa kufuatia kuondoka kwa mlinda lango nambari wani wa klabu hiyo David De Gea, Mason Mount kutoka Chelsea pamoja na Rasmus Hojlund.

Manchester United watakuwa na kibarua Agosti 14 ugani Old Trafford, watakapokuwa wakikabiliana na Wolves katika mechi ya kwanza msimu mpya wa ligi kuu Uingereza.