Wakenya wapagawa EPL wakitumia lugha ya sheng' FB kutangaza ujio wa ligi ya premia

EPL inang'oa nanga wikendi hii na mchuano kati ya Liverpool na Chelsea ndio mkubwa kwa mechi zote. PL waliupigia debe mchuano huu wakitumia Kiswahili-sheng' cha Kenya.

Muhtasari

• Tangazo hilo liikuwa linawarai Wakenya kutokosa kufuatilia mchuano huo na badala yake kuupata moja kwa moja kwenye ving'amuzi vya GOtv.

Tangazo la EPL kwa Sheng'
Tangazo la EPL kwa Sheng'
Image: FACEBOOK

Wakenya wapenzi wa soka na haswa ligi kuu ya Uingereza EPL walibaki vinywa wazi baada ya ukurasa wa ligi kuu ya EPL kwenye mtandao wa Facebook kuandika tangazo la ujio wa ligi mpya msimu 2023/24 kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Ukurasa wa Premier League wenye wafuasi milioni 46 na ambao umethibitishwa kwa kukabidhiwa alama ya bluu ya Meta uliandika tangazo hilo kwa Kiswahili cha Kenya wakati wanatangaza mechi moja kubwa kati ya mechi zote za ligi ya premia ambazo zitang’oa nanga wikendi hii.

Premier League walitangaza mechi ya Chelsea na Liverpool huku wakipigia debe Wakenya kupata pambano hilo kubwa kupitia ving’amuzi vya GOtv humu nchini.

Chelsea watapea Liverpool ‘The Blues’ ama watakuwa humbled by The Reds na 3 points ziwe snatched from them? ” Tangazo hilo lilisoma.

Hili liliwapunga Wakenya ambao walifurika na kuachia maoni mbali mbali wengine wakionekana kustaajabu nani huyo aliyefunza msimamizi wa ukurasa huo Kiswahili – kwani inaaminiwa wanaofanya kazi kwenye ligi kuu ya EPL wengi si kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambako Kiswahili ni lugha ya kuwaunganisha wenyewe wa upande huo wa Afrika.

Wengine walidai kwamba ukurasa huo umedukuliwa na wengine wakisema ni wasimamizi wa GOtv ambao walilipia tangazo hilo kwenye ukurasa wa PL na kuandika ujumbe ambao walitaka uandikwe pale.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa Wakenya;

“Hongera sana kutoka Kenya. Sikujua sisi ni wakubwa hivi” Ronald Ng’etich Kimutai.

“And that's why I love Kenyans.... Yaani mko kote, hadi hii page mkanyakua nyakunyaku,” Wuon Bongu.

“I thought hi page ni eppll ya majuu,” mwingine alisema.

“Yaani looks premier league mmetuamulia ni shembeteng nayo nayo” Provesa Nyox.

“Kwahiyo Mkenya amekuwa akiendesha ukurasa huu aki weeeh.” Mwingine aling’aka.

Angalia tangazo hili kutoka kwa ukurasa huo rasmi wa PL;

EPL, CHELSEA, LIVERPOOL
EPL, CHELSEA, LIVERPOOL