Neymar akiri mchango mkubwa wa Ronaldo kuwavutia wanasoka kwenda Saudi Arabia

''Naamini Cristiano Ronaldo alianza haya yote na kila mtu alimwita 'kichaa', na hili na lile, leo unaona ligi zaidi na zaidi,'' Neymar.

Muhtasari

• Huku Ronaldo, Neymar, Karim Benzema, N'Golo Kane na Jordan Henderson baadhi tu ya majina ambayo yametua Uarabuni.

Neymar na Ronaldo
Neymar na Ronaldo
Image: Instagram

Kufuatia kukamilika kwa uhamisho wake wa hivi majuzi wa kwenda Al-Hilal, fowadi mwenye umri wa miaka 31 Neymar amesisitiza mengi anastahili heshi kubwa fowadi wa Al-Nassr Ronaldo, kwa ushawishi wake katika ukuaji wa hivi majuzi wa soka nchini Saudi Arabia.

Neymar alikamilisha uhamisho wake wa kihistoria kwa mara nyingine tena kwenda Al Hilal akitokea miamba wa Ufaransa PSG.

''Naamini Cristiano Ronaldo alianza haya yote na kila mtu alimwita 'kichaa', na hili na lile, leo unaona ligi zaidi na zaidi,'' Neymar alikiambia kituo rasmi cha Al-Hilal, kufuatia uhamisho wake kutoka Paris Saint-Germain.

Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona atalipwa kitita cha pauni milioni 137 ($174m/€160m) nchini Saudi Arabia.

Huku Ronaldo, Neymar, Karim Benzema, N'Golo Kane na Jordan Henderson baadhi tu ya majina ambayo yamebadilisha ligi zinazoongoza Ulaya kwenye jimbo la Ghuba msimu huu wa joto, kuna uwezekano bado tutaona wachezaji wengi zaidi wakielekea Saudi Pro League miaka inayofuata.

Huku ikiwa bado haijathibitishwa ni lini mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ataanza kucheza kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo, Al-Hilal itacheza Jumamosi hii, huku kikosi cha Jorge Jesus kikimenyana na Al-Feiha siku ya Jumamosi.

Ronaldo ndiye alikuwa mchezaji staa mkubwa wa kwanza kugura ligi za juu za mataifa ya Ulaya na kuchagua kwenda Saudi Arabia Januari mwaka huu, uhamisho ambao alisema tayari yeye ameshakamilisha kila kitu katika ligi za Ulaya.

Taifa la Saudi Arabia limefanya usajili mkubwa wa wachezaji kwenye timu zake katika mbinu ambayo inaonekana kutoa mchango mkubwa kwenye soka na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kutoa ombi kwa FIFA kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2032.