• Mchapishaji wa video hiyo kutoka Brazil alisema kwamba walikuwa wanafanya hivyo ili kumfunga Neymar asije akawafunga na kuwabamiza.
Siku moja baada ya mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya wenyeji Peru na wageni Brazil kukamilika kwa ushindi mwembamba wa Brazili kwa bao la Marquinhos, sasa video moja imeibuka mitandaoni ikionesha watu waliokuwa kama waganga wa Peru wakifanya ushirikina kwa Neymar ili asiwafunge bao katika mecho hiyo.
Inaaminika kwamba baada ya kuona Brazili ikiirindima Bolvia mabao 5-1 na kuvuna ushindi mnono katika mecho ambayo Neymar alitikiza wavu mara mbili, wapenzi wa soka kutoka Peru waliingiwa na mchecheto na kuamua kutafuta mbinu ya kumzuia Neymar kuwabamiza.
Watu hao wanaokisiwa kuwa waganga wa kiasili wanaweza kuonekana kwenye video hiyo wakicheza densi za kilingeni huku wakiikanyaga picha ya Neymar barabarani wakiwa wanatamka maneno yasiyosikika.
Mchapishaji wa video hiyo kutoka Brazil alisema kwamba walikuwa wanafanya hivyo ili kumfunga Neymar asije akawafunga na kuwabamiza.
Hata hivyo, ushirikina huo wao ulionekana kutofua dafu kwa ufanisi mkubwa baada ya Brazil kuichabanga Peru bao 1-0 lililofungwa na nahodha wa PSG, Marquinhos na asisti ya bao hilo ilitokana na Neymar mwenyewe.
Wakati huo huo, kocha wa Brazil Fernando Diniz amempongeza Neymar kwa kuvunja rekodi ya Pele, ambayo ilikuwa imesimama kwa miongo kadhaa.
Neymar, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, anasalia kuwa mchezaji muhimu wa Brazil licha ya kujiunga na Al Hilal ya Saudi Arabia katika majira ya joto.
Tazama video hiyo haya chini;