Odegaard asaini mkataba mpya wa miaka mitano Arsenal

Odegaard, ambaye pia ni nahodha wa Norway amecheza mechi 53

Muhtasari

Alishiriki katika mechi zote isipokuwa moja kati ya mechi 38 za Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita huku vijana wa Mikel Arteta wakimaliza washindi wa pili baada ya Manchester City.

Odegaard, ambaye pia ni nahodha wa Norway  amecheza mechi 53, amejitolea kuitumikia Arsenal hadi mwisho wa msimu wa 2027-28.

Nahodha wa Asernal Martin Odegaard
Nahodha wa Asernal Martin Odegaard
Image: Twitter

  Nahodha wa Arsenal Martin Odegaard amesaini mkataba mpya wa miaka mitano,Kiungo huyo wa kati wa Norway,  amefunga mabao 27 na kutoa asisti 15 katika mechi 112 alizoicheza

 Odegaard alijiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid mnamo Agosti 2021 kwa takriban pauni 30m kufuatia mkopo .

Alishiriki katika mechi zote isipokuwa moja kati ya mechi 38 za Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita huku kikosi cha Mikel Arteta kilimaliza washindi wa pili baada ya  Manchester City na kumaliza miaka sita ya kutoshiriki Ligi ya Mabingwa.

"Kusaini mkataba mpya ulikuwa uamuzi rahisi kwangu kwa sababu nyingi," Odegaard alisema. Hasa kile tunachofanya hivi sasa kama klabu ni kuweka rekodi mpya na ninataka kuwa sehemu ya hiyo rekodi.

Odegaard, ambaye pia ni nahodha wa Norway amecheza mechi 53, amejitolea kuitumikia Arsenal hadi mwisho wa msimu wa 2027-28.

Amefunga mabao matatu katika mechi saba alizoichezea Arsenal msimu huu - ikiwa ni pamoja na bao zuri siku ya Jumatano wakati klabu hiyo ikirejea kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya PSV Eindhoven.

Alijiunga na wababe hao wa Uhispania akiwa na umri wa miaka 16 kutoka klabu ya Stromsgodset ya Norway mwaka 2015, na kuwa mchezaji mdogo zaidi Real Madrid .

Hayo yalikuja baada ya kuwa mchezaji wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 15 na siku 253 alipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Falme za Kiarabu.

Odegaard alitatizika kutulia Bernabeu na alikuwa na muda wa mkopo katika vilabu vya Uholanzi Heerenveen na Vitesse, na Real Sociedad ya Uhispania, kabla ya kuwasili London kaskazini Januari 2021.