Harry Kane akutana na mtu anayeonekana zaidi kama Harry Kane kuliko Harry Kane mwenyewe

Kwa mujibu wa jarida la Daily Star, Steffen amekuwa akivalia kama yeye tangu kuwasili kwake majira ya joto kutoka Tottenham.

Muhtasari

• Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alivaa Lederhosen ya kitamaduni na kunywea stein.

• Alikutana kwa ghafla na jamaa aliyetambulika kama Steffen ambaye wanafanana kama shilingi kwa ya pili.

Harry Kane na 'pacha wake'
Harry Kane na 'pacha wake'
Image: Screengrab

Nyota wa Bayern Munich Harry Kane alikutana ana kwa ana na ‘pacha wake’ wa Kijerumani alipokuwa akisherehekea Oktoberfest.

Akiwa amevalia nadhifu baada ya kufunga hat-trick yake ya kwanza ya Bundesliga katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Bochum, Kane alijitumbukiza katika sherehe za kila mwaka za kunywa bia na wachezaji wenzake Manuel Neuer na Thomas Muller pamoja na meneja Thomas Tuchel Jumapili (Septemba 24).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alivaa Lederhosen ya kitamaduni na kunywea stein - huku pia akikutana kwa ghafla na jamaa aliyetambulika kama Steffen ambaye wanafanana kama shilingi kwa ya pili.

Kwa mujibu wa jarida la Daily Star, Steffen amekuwa akivalia kama yeye tangu kuwasili kwake majira ya joto kutoka Tottenham. Walipiga picha ya pamoja kwa mara ya kwanza.

Kane, ambaye timu yake ya zamani ilikuwa ikipigana vikali kwa sare ya 2-2 kaskazini mwa London derby huku akiwa na shughuli nyingi za kubugia, bila shaka amekuwa akifurahia maisha nje ya Uingereza hadi sasa.

Amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga mabao sita au zaidi katika mechi tano za kwanza za Bundesliga kwa mabao yake saba, pamoja na kusajili mabao manne katika mashindano yote.

Tuchel alijawa na sifa tele baada ya ushindi wao wa 4-3 wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United wiki iliyopita, ambapo Kane pia alifunga papo hapo. Alisema: "Ni jambo kubwa, tulimtoa nahodha wa England kutoka England.