Majeruhi wa Ligi Kuu - 'Wachezaji hawawezi tena kukabiliana na mzigo huu uliokithiri'

Timu 20 za Ligi kuu za Uingereza kwa sasa zina jumla ya wachezaji 112 ambao wamejeruhiwa.

Muhtasari

•Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anafikiri wachezaji wanapaswa kukusanyika ili kulazimisha mabadiliko ya ratiba.

Image: BBC

"Wachezaji hawawezi tena kukabiliana na mzigo huu."

Hayo ni maneno ya kusikitisha ya Erik ten Hag wakati meneja wa Manchester United akipambana na orodha inayoongezeka ya majeruhi.

Mholanzi huyo alikuwa akizungumza siku ambayo mlinzi wake Lisandro Martinez alitolewa nje hadi mwisho wa mwisho , na hivyo kufanya jumla ya wachezaji wasiokuwepo United kufikia wanane.

Lakini Ten Hag sio meneja pekee wa Premier League ambaye atakabiliwa na orodha ndefu ya majeruhi wiki sita tu baada ya msimu mpya.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anafikiri wachezaji wanapaswa kukusanyika ili kulazimisha mabadiliko ya ratiba.

Meneja wa Newcastle Eddie Howe, meneja wa Arsenal Mikel Arteta na mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino pia wamekuwa na maoni yao kuhusu suala hilo.

Kulingana na PremierInjuries.com, Timu 20 za Ligi kuu za Uingereza kwa sasa zina jumla ya wachezaji 112 ambao wamejeruhiwa.