Mechi ya Uholanzi yasimamishwa baada ya kipa kupoteza fahamu

Wachezaji walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati Vaessen akiwa kimya akipatiwa matibabu uwanjani

Muhtasari

•Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 84 baada ya Mholanzi huyo, 28, kugongana na mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey.

Image: BBC

Mechi ya vinara wa Uholanzi kati ya RKC Waalwijk na Ajax iliachwa baada ya kipa wa Etienne Vaessen kupoteza fahamu.

Mchezo huo ulisimamishwa katika dakika ya 84 baada ya Mholanzi huyo, 28, kugongana na mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey.

Wachezaji walitaka usaidizi kwa hamaki na walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati Vaessen aliyekuwa kimya akipatiwa matibabu uwanjani, na skrini iliyowekwa ikionyesha kinachojiri.

Klabu yake ilisema alipata fahamu wakati akitolewa kwenye machela. RKC alisema: “Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kimatibabu amesafirishwa hadi hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Ajax walikuwa wakiongoza mchezo wa Jumamosi wa Eredivisie kwa mabao 3-2 kabla ya mechi kusimamishwa.