Kiungo wa Arsenal Mohammed Elneny aanzisha klabu yake baada ya kusahaulika na Arteta

"Lengo langu ni kufikia ndoto za wachezaji watoto na kuboresha uchezaji wao katika kandanda pamoja na kuwasaidia kufikia kiwango cha juu."

Muhtasari

• Elneny FC itatoa njia iliyopangwa kwa vijana wenye vipaji wenye umri wa miaka 5-16 na 16-25 kubadili kutoka kwa soka isiyo ya ligi hadi safu ya kulipwa.

Mohammed Elneny.
Mohammed Elneny.
Image: Instagram

Kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny amezindua klabu yake ya soka, jarida la London World limesema.

Elneny FC itatoa njia iliyopangwa kwa vijana wenye vipaji wenye umri wa miaka 5-16 na 16-25 kubadili kutoka kwa soka isiyo ya ligi hadi safu ya kulipwa.

Maono ya akademia ni ya moja kwa moja: kuziba pengo kati ya soka ya ngazi ya chini na ya kulipwa, na akademi hiyo ikikuza talanta mapema kama miaka 5 na , ikiendelea kuongoza maendeleo yao wanapofikisha miaka 16.

Mchezaji wa kimataifa wa Misri Elneny, ambaye ana leseni B ya UEFA, anashiriki kikamilifu katika baadhi ya vikao vya kufundisha, akileta uzoefu wake mkubwa kama mchezaji wa Ligi Kuu ili kunufaisha vipaji vya vijana.

Kwa kutoa mwongozo uliopangwa, utaalamu wa kufundisha, na kujitolea bila kuyumbayumba, analenga kuunda mustakabali wa maendeleo ya soka, jarida hilo lilisema.

"Lengo langu ni kufikia ndoto za wachezaji watoto na kuboresha uchezaji wao katika kandanda pamoja na kuwasaidia kufikia kiwango cha juu."