Mbibu na mbichi kujulikana Simba SC ikiwakaribisha Al Ahly African Football League

Leo Mashabiki wataburudishwa kwa mchuano wa kumezea mate baina ya wenyeji Simba SC na miamba wa soka wa Misri Al Ahly.

Muhtasari

• Taarifa za ndani zinasema rais wa FIFA Gianni Infantino na aliyekuwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger watakuwepo kufungua kipute hicho.

African Football League
African Football League
Image: Instagram

Ligi ya vilabu vya soka barani Afrika, kwa kimombo African Football League itang’oa nanga nchini Tanzania kuanzia leo Ijumaa Oktoba 20.

Ligi hiyo inazinduliwa katika uwanja wa kimataifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na itajumuisha vilabu 8 vikiwemo Simba SC ya Tanzania, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, miamba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, TP Mazembe, Petro Atletico de Luanda ya Angola, Esperance ya Tunisia, Al Ahly ya Misri, Enyimba ya Nigeria na Wydad ya Morocco.

Leo Mashabiki wataburudishwa kwa mchuano wa kumezea mate baina ya wenyeji Simba SC na miamba wa soka wa Misri Al Ahly.

Shindano hilo lilizinduliwa mwaka jana, likiwa na zawadi ya dola milioni 4 kwa washindi.

Katika ufunguzi wa kinyang'anyiro hicho, msanii Alikiba atakuwa mmoja wa wasanii wakubwa watakaotumbuiza majira ya saa kumi na mbili thenashara.

Taarifa za ndani zinasema rais wa FIFA Gianni Infantino na aliyekuwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger watakuwepo kufungua kipute hicho.