•Vini Jr alibainisha kuwa alifanyiwa ubaguzi wa rangi na msichana mdogo ambaye alihudhuria mechi hiyo ya Jumamosi jioni iliyoisha kwa sare ya 1-1.
•"Ni huzuni sana hakuna wa kumsomesha. Ninawekeza, na ninawekeza sana, katika elimu nchini Brazil ili kuwafunza raia wenye mitazamo tofauti," alisema.
Mshambulizi wa Real Madrid Vinicius Junior amelalamikavikali hadharani baada ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi wakati wa mchuano wao dhidi ya Sevilla kwenye uwanja wa Estadio Ramon Sanchez Pizjuan siku ya Jumamosi jioni.
Katika taarifa aliyochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 23 alibainisha kuwa alifanyiwa ubaguzi wa rangi na msichana mdogo ambaye alihudhuria mechi hiyo ya Jumamosi jioni iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Vinicius Jr alilalamika kwamba msichana huyo mdogo aliyemnyanyasa hakupata elimu ifaayo kuhusu jinsi ya kutenda maadili.
"Hongera Sevilla kwa nafasi ya haraka na penalti katika kipindi kingine cha kusikitisha kwa Soka ya Uhispania. Kwa bahati mbaya nimepata video ya kitendo kingine cha ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa Jumamosi hii, safari hii kikifanywa na mtoto,” Vinicius Jr alilalamika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Aliongeza, “Ni huzuni sana hakuna wa kumsomesha. Ninawekeza, na ninawekeza sana, katika elimu nchini Brazil ili kuwafunza raia wenye mitazamo tofauti.”
Shirika la Kimataifa la Brazil limelaani kitendo cha ubaguzi wa rangi kilichoonyeshwa na mashabiki wa Sevilla na kuwataka viongozi wa soka wa Uhispania kuhakikisha adhabu inatolewa kwa wahusika.
Vini Jr hata alijitolea kusaidia katika kutokomeza ubaguzi wa rangi katika kandanda kabla ya Kombe la Dunia la 2030 ambalo litafanyika Uhispania, Brazil na Morocco.
"Uso wa wabaguzi wa rangi wa leo umebandikwa kwenye tovuti kama mara nyingine kadhaa. Natumai mamlaka ya Uhispania itafanya sehemu yao na kubadilisha sheria mara moja na kwa wote. Watu hawa pia wanahitaji kuadhibiwa kwa jinai. Itakuwa hatua nzuri ya kwanza kujiandaa kwa Kombe la Dunia la 2030. Niko hapa kusaidia. Samahani kwa sauti inayojirudia lakini ni sehemu namba 19. Na kuhesabu ... ✊���,” alisema.
Katika video iliyoifikia Radio Jambo, msichana mdogo katika miaka yake ya ujana anaonekana akifanya mitindo ya tumbili huku wachezaji wa Real Madrid na Sevilla wakipambana uwanjani.
Vinicius Jr mwenye ghadhabu kweli anaonekana kuwakabili baadhi ya mashabiki waliosimama kwenye viti ambao wanaonekana kumuudhi. Mwenzake Jude Bellingham kisha anaonekana akimpoza na kumrudisha uwanjani.