Aliyekuwa kiungo wa Nigeria Jay Jay Okocha asherehekea miaka 25 kwenye ndoa

Katika video nyingine ya kusisimua, mke mrembo wa Jay Jay Okocha, Nkechi, alivalia gauni maridadi jeusi huku wawili hao wakicheza kwa furaha karibu na kila mmoja.

Muhtasari

• Watoto wao wawili wa kupendeza, Ajay Okocha na Daniela Okocha, pia walikuwepo kushiriki furaha yao.

Jay Jay Okocha
Jay Jay Okocha
Image: Instagram

Kiungo wa kati matata wa timu ya taifa ya Nigeria miaka ya 90 na mapema 2000s Jay Jay Okocha alifanya tafrija ya kipekee kusherehekea kufikisha miaka 50 na pia kusherehekea miaka 25 kati ya hiyo akiwa ndani ya ndoa na mkewe, Nkech.

Mkwasi huyo wa kupiga chenga za kimaudhi alisherehekea matukio haya mwili kwa pamoja katika mji wa kimahaba wa Maldives kwa karamu iliyoenea mitandaoni.

Video kutoka kwa tukio hilo la kushangaza zilivutia watu wengi, zikiangazia mitandao ya kijamii.

Wawili hao walionekana wakirejesha viapo vyao katika hafla ya kugusa hisia ambapo walionekana kustaajabisha wakiwa wamevalia vazi jeupe la kitamaduni la arusi.

Katika video nyingine ya kusisimua, mke mrembo wa Jay Jay Okocha, Nkechi, alivalia gauni maridadi jeusi huku wawili hao wakicheza kwa furaha karibu na kila mmoja.

Watoto wao wawili wa kupendeza, Ajay Okocha na Daniela Okocha, pia walikuwepo kushiriki furaha yao.