Thierry Henry afunguka kuhusu msongo wa mawazo wakati wa taaluma yake ya soka

Anasema kulikuwa na kipindi mapema katika janga la corona ambapo "alikuwa akilia karibu kila siku".

Muhtasari

•Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 alifunga rekodi ya klabu mabao 228 katika michezo 377 akiwa na The Gunners.

•Henry alisema uhusiano wake na babake, ambaye anasema alikuwa mkosoaji wa uchezaji wake, unaweza kuwa na athari kwake.

Image: BBC

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anasema "lazima awe alikuwa na huzuni" wakati wa uchezaji wake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 alifunga rekodi ya klabu mabao 228 katika michezo 377 akiwa na The Gunners na kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998 na Euro 2000 akiwa na Ufaransa.

"Katika kazi yangu yote, na tangu nilipozaliwa, lazima ningekuwa katika msongo wa mawazo," Henry aliambia Diary of a CEO podcast.

"Je! nilijua? Hapana. Je! nilifanya kitu juu yake? Hapana. Lakini nilijizoea kwa njia fulani."

Henry sasa ni mkufunzi wa Vijana wa U-21 wa Ufaransa, pia alifanya kazi kwenye benchi Ła ukocha wa Ubelgiji na aliisimamia Monaco kabla ya kuchukua mikoba ya Montreal Impact mwishoni mwa 2019.

Anasema kulikuwa na kipindi mapema katika janga la corona ambapo "alikuwa akilia karibu kila siku".

"Lazima uweke mguu mmoja [mbele] na mwingine na utembee," alisema.“Hivyo ndivyo nilivyoambiwa tangu nikiwa mdogo.

"Sikuacha kutembea - [kama ningefanya] basi labda ningetambua [kuhusu matatizo ya kiafya]. Wakati wa Covid - Niliacha kutembea. Sikuweza. Kisha unaanza kutambua."

Mshambulizi huyo wa zamani wa Juventus, Monaco na Barcelona aliongeza: "Nilikuwa peke yangu huko Montreal, na kutoweza kuwaona watoto wangu kwa mwaka mmoja ilikuwa ngumu.

"Machozi yalikuwa yanatirirka . Mbona sijui, lakini labda walikuwa huko kwa muda mrefu sana."

Henry alisema uhusiano wake na babake, ambaye anasema alikuwa mkosoaji wa uchezaji wake, unaweza kuwa na athari kwake.

Alisema baba yake "alikuwa na mani yen makali sana nyakati fulani kuhusu jinsi nilivyokuwa mchezaji".

"Kama mvulana mdogo ilikuwa daima 'hukufanya vizuri'," alisema.

"Kwa hivyo ni wazi unaposikia kwamba mara nyingi zaidi kuliko sivyo, hiyo ndiyo itasalia."