Tuko mbioni kushindania mataji ya EPL na FA - Ten Hag baada ya Man Utd kupiga Wigan

Pia waliondolewa kwenye Kombe la Carabao na Newcastle United, kombe lilelile waliloshinda msimu uliopita kwa kuifunga Newcastle katika fainali uwanjani Wembley

Muhtasari

• Mashetani Wekundu walitupwa nje ya Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza mkia kwenye kundi lao, nyuma ya Bayern Munich, FC Copenhagen, na Galatasaray.

• Pia waliondolewa kwenye Kombe la Carabao na Newcastle United, kombe lilelile waliloshinda msimu uliopita kwa kuifunga Newcastle katika fainali uwanjani Wembley.

Erik Ten Hag
Erik Ten Hag
Image: Manchester United

Meneja wa Manchester United, Erik Ten Hag hajafutilia mbali matumaini ya kushinda ligi kuu ya premia msimu huu licha ya timu yake kusuasua katika mkondo wa kwanza wa ligi hiyo yenye ushindani mkali.

Akizungumza baada ya Manchester United kuipiga Wigan katika raundi ya 3 ya kombe la FA, Ten Hag alisema kwamba United bado wako kwenye kinyang’anyiro cha mataji mawili – ligi kuu ya premia na FA na watahakikisha wameibuka kama mabingwa katika vinyang’anyiro hivyo.

“Bado tuna Ligi Kuu, hivyo tuna mataji mawili ya kuchezea. Tutachezea Ligi Kuu na Kombe la FA,” Ten Hag alisema.

Manchester United imekuwa na sintofahamu, ikipata hasara ya kushtukiza dhidi ya Bournemouth na Nottingham Forest, bado imepata ushindi dhidi ya Aston Villa na Chelsea.

Mashetani Wekundu walitupwa nje ya Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza mkia kwenye kundi lao, nyuma ya Bayern Munich, FC Copenhagen, na Galatasaray.

Pia waliondolewa kwenye Kombe la Carabao na Newcastle United, kombe lilelile waliloshinda msimu uliopita kwa kuifunga Newcastle katika fainali uwanjani Wembley.

Ili kuwaongezea masaibu, wamo katika nafasi ya nane kwenye jedwali la Ligi Kuu wakiwa na pointi 31 - pointi 14 kutoka kileleni baada ya raundi 20.

Manchester United walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Wigan Athletic katika raundi ya tatu ya Kombe la FA, na kutinga katika raundi ya nne.

Diogo Dalot na Bruno Fernandes walifunga kila kipindi, huku Dalot akifunga bao dakika ya 22 na Fernandes akifunga penalti dakika ya 74 baada ya kuchezewa vibaya na Liam Shaw.