Wanigeria wakosolewa kwa kumshambulia mtandaoni Iwobi baada ya kushindwa Afcon

Baadhi ya mashabiki wanamlaumu kiungo Alex Iwobi kwa kushindwa na Nigeria kwenye Afcon

Muhtasari

•Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Nigeria, Super Eagles ameongoza wito wa kukomesha unyanyasaji wa mtandaoni dhidi ya kiungo Alex Iwobi.

•Mashambulizi hayo ya mtandaoni yalimfanya Iwobi kufuta picha zake za Instagram siku ya Jumatatu.

Baadhi ya mashabiki wanamlaumu kiungo Alex Iwobi kwa kushindwa na Nigeria kwenye Afcon
Baadhi ya mashabiki wanamlaumu kiungo Alex Iwobi kwa kushindwa na Nigeria kwenye Afcon
Image: BBC

Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Nigeria, Super Eagles ameongoza wito wa kukomesha unyanyasaji wa mtandaoni dhidi ya kiungo Alex Iwobi.

Baadhi ya mashabiki wa soka wamekuwa wakimnyanyasa Iwobi kwenye mitandao ya kijamii, wakimlaumu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kufungwa mabao 2-1 na Ivory Coast katika michuano ya fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika ( Afcon)Jumapili.

Iwobi alicheza kwenye mechi hiyo kwa dakika 79, kabla ya kuondolewa na Alhassan Yusuf.

Mashambulizi hayo ya mtandaoni yalimfanya Iwobi kufuta picha zake za Instagram siku ya Jumatatu.

Nahodha wa Super Eagles Ahmed Musa na baadhi ya Wanigeria wengine wamefmtetea Iwobi, na kulaani mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya mchezaji huyo na kusema si haki kumtenga kwa kupoteza timu.

"Wapenzi mashabiki, nataka kuwasihi msitishe uonevu mtandaoni unaoelekezwa kwa Alex Iwobi," Musa alishiriki kwenye X, zamani Twitter.

"Kushindwa bila shaka ni ngumu, lakini kumlenga mchezaji mmoja kwa mapungufu ya timu sio haki na sio haifai. Tunashinda kama timu, na tunapoteza kama timu. Alex alijitolea uwanjani, kama kila mshiriki wa kikosi chetu. ," aliongeza.

Iwobi bado hajatoa tamko lolote kuhusu mashambulizi dhidi yake.