logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kanye West akashifiwa kwa kudai anatamani mapenzi ya watatu na Michelle Obama (video)

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Wet kuonekana kuvutiwa na Michelle Obama.

image
na Radio Jambo

Football23 April 2024 - 08:13

Muhtasari


• Michelle Obama alikuwa Mke wa Rais wa Marekani kuanzia 2009-2017 - akiwa ameolewa na rais wa zamani Barack Obama.

Kanye West

Kanye West amefichua ni mtu mashuhuri gani yeye na mkewe Bianca Censori wanaweza kumkaribisha katika chumba chao cha kulala kwa ajili ya mapenzi kwenye mahojiano yake ya hivi punde ya kushangaza.

Siku chache tu baada ya rapper West kutajwa kuwa mtuhumiwa wa kumshambulia mtu baada ya tukio huko Los Angeles, nyota huyo, 46, alizungumza juu ya maisha yake ya kimapenzi katika mazungumzo ya wazi na podikasti ya Download.

Akiwa anang'arisha meno yake ya titanium, rapper huyo alionekana kuwa na mawazo tele huku akiulizwa na mtangazaji Justin Laboy ni mwanamke gani maarufu angependa kukutana naye kwa mapenzi ya watatu - kabla ya kujibu: 'Michelle Obama!'

Kisha akaongeza: 'Unapaswa kukutana na mke wa Rais!'

Michelle Obama alikuwa Mke wa Rais wa Marekani kuanzia 2009-2017 - akiwa ameolewa na rais wa zamani Barack Obama.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Wet kuonekana kuvutiwa na Michelle Obama.

Mnamo 2013, West alizua ghasia baada ya kudai kwamba mchumba wake Kim Kardashian alikuwa na ushawishi zaidi kuliko Michelle.

Alisema: 'Hakuna jinsi Kim Kardashian asiwe kwenye jalada la Vogue. Yeye ni kama mwanamke anayevutia zaidi kwa sasa.’

'Na kwa pamoja, sisi ndio wenye ushawishi mkubwa katika mavazi. Hakuna anayeangalia kile [Barack Obama] amevaa. Michelle Obama hawezi weka picha [ya bikini] Instagram kama vile msichana wangu alifanya juzi kati.'

Haya yanajiri baada ya mwanamuziki huyo kugombana na mwanamume mkewe Censori, 29, akidai kumdhulumu kimwili na kingono katika ukumbi wa Chateau Marmont siku ya Jumatano.

Hata hivyo, ungamo hilo halikuenda vyema kwa baadhi ya watu ambao walihisi Kanye West anamkosea heshima mama taifa wa zamani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved