logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Refa apigwa marufuku ya maisha kutojihusisha na soka

Mwamuzi wa soka ,John Smit amepigwa marufuku ya maisha ya kutojihusisha na masuala ya soka.

image
na Radio Jambo

Football17 May 2024 - 07:22

Muhtasari


•Mwamuzi Jan Smit kutoshiriki tena katika masuala ya Soka.

•FA ya Uholanzi,KNVB yamwachisha kazi mwamuzi,Jan Smit.

picha;twitter

Refa wa daraja la nne nchini Uholanzi amepigwa marufuku kutojihusisha na masuala ya soka .

Jan Smit mwenye umri wa miaka 61 , anayetoka Opmeer kaskazini mwa Uholanzi alisimamia mechi kati ya St.George na SV De Valken siku ya Jumapili 12,Mei 2024.

Mchezo huo ulishuhudia mlinda lango wa St.George,Dave Laan akifunga bao la ushindi dakika za lala salama.Hii ilionekana kusaidiwa na vitendo vya Smit kwa kuongeza  dakika 15 .SV De Valken walionyeshwa kadi tatu nyekundu na moja kwa mkufunzi wa benchi la ufundi.Baada ya mechi,video ilisambazwa mtandaoni ikionyesha Smit akisherehekea na wachezaji wa St.George.

Klabu ya De Valken iliwasilisha malalamiko yao dhidi ya mwamuzi huyo.Hapo awali alisimamishwa  mwaka ,2021  kwa "tabia isiyofaa". Na FA ya Uholanzi, KNVB, sasa imempa marufuku ya maisha baada ya tukio hilo.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa KNVB Daan Schippers ilisema:

 

 'Tumepokea malalamiko kadhaa baada ya mechi ya Jumapili. Leo asubuhi tulimpigia simu Bw Smit na kumwambia kwamba haruhusiwi tena kuchezesha mechi za waamuzi. Tunatarajia mtazamo wa kutoegemea upande wowote kutoka kwa mwamuzi na kwamba timu zote mbili zitatendewa kwa heshima. Hapo ndipo ambapo mtazamo huu unafaa.'

Lakini Smit amejibu uamuzi huo kwa kusisitiza  kuwa hana makosa. Akizungumza na NH Nieuws, alisema:

"Sikusherehekea na wachezaji hata kidogo. Niliimba tu wimbo na kuinua kombe mara moja. Hilo ndilo jambo pekee.Naona huzuni sana kwa maneno kwamba KNVB wananiondoa kwa sababu hiyo. Inachekesha kwa kuwa KNVB haijafanya utafiti wowote na imetazama video moja pekee.Nadhani kwamba kupiga firimbi sasa kumekwisha, lakini sitapiga magoti tena kama nilivyofanya miaka miwili iliyopita."

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved