logo

NOW ON AIR

Listen in Live

EPL 2024/25: Chelsea kuanza msimu dhidi ya Man City, Arsenal vs Wolves, Man U vs Fulham...

Jumatatu ya Agosti 19, malimbukeni Leicester City watamaliza udhia dhidi ya Tottenham Hotspurs.

image
na Davis Ojiambo

Michezo18 June 2024 - 08:32

Muhtasari


  • • Mechi zingine kwenye Jumamosi hiyo zitakuwa ni Arsenal dhidi ya Wolves, Everton dhidi ya Brighton, Newcastle dhidi ya Southampton, Nottingham Forest dhidi ya Bournemouth na Westham dhidi ya Aston Villa kufunga siku.

Ratiba ya msimu mpya wa mwaka 2024/25 kwenye ligi kuu ya Premia nchini Uingereza imetolewa rasmi.

Ligi hiyo itang’oa nanga Ijumaa ya Agosti 16 ambapo Manchester United watawakaribisha Fulham ugani Old Trafford.

Wikendi ya kwanza ya msimu ambayo itakuwa Jumamosi ya Agosti 17 itashuhudia mechi ya mapema mwendo wa saa tisa mchana kati ya malimbukeni Ipswich wakiwakaribisha Liverpool.

Mechi zingine kwenye Jumamosi hiyo zitakuwa ni Arsenal dhidi ya Wolves, Everton dhidi ya Brighton, Newcastle dhidi ya Southampton, Nottingham Forest dhidi ya Bournemouth na Westham dhidi ya Aston Villa kufunga siku.

Jumapili ya kwanza ya msimu itashuhudia mechi kubwa ambapo Chelsea watakaribisha mabingwa watetezi Manchester City gani Stamford Bridge.

Jumatatu ya Agosti 19, malimbukeni Leicester City watamaliza udhia dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Hii hapa ratiba kamili ya msimu mpya’

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved