Man Utd ni kama Coca-Cola, kila mtu duniani anaijua! – Jim Ratcliffe, mmiliki mwenza

Ratcliffe alisema kwamba kwa sasa lengo lao ni kuifanya Man Utd kuwa kama Real Madrid na kwamba hilo litahitaji madirisha ya uhamisho kama 3 pekee kufikia malengo yao.

Muhtasari

• Ratcliffe alisema kwamba kwa sasa lengo lao ni kuifanya Man Utd kuwa kama Real Madrid na kwamba hilo litahitaji madirisha ya uhamisho kama 3 pekee kufikia malengo yao.

JIM RATCLIFFE
JIM RATCLIFFE
Image: x

Mmiliki wa hisa zilizo chache katika klabu ya soka ya Manchester United ameutaja umaarufu wa klabu hiyo duniani kama ule wa inywaji cha Coca Cola.

Akizungumza na Bloomberg, Jim Ratcliffe alisema kwamba klabu hiyo ni maarufu kote duniani na kudai kila mtu anautambua mji wa Manchester kutokana na ufanisi wa klabu hiyo.

“Kila mtu duniani anaujua mji wa Manchester kwa sababu ya Manchester United. Klabu hii ni kama Coca-Cola, si ni hivyo? Kila mtu anaijua. Sina uhakika ni kwa nini lakini huo ndio ukweli,” Ratcliffe alisema.

Kuhusu mipango yake katika mustakabali wa kurejesha klabu hiyo kwenye njia yake ya ufanisi, Ratcliffe alisema  kuwa kuna mabadiliko mengi ambayo wameyaandaa na katika miaka michache ijayo, wanataka kufanikiwa.

Ratcliffe alisema kwamba kwa sasa lengo lao ni kuifanya Man Utd kuwa kama Real Madrid na kwamba hilo litahitaji madirisha ya uhamisho kama 3 pekee kufikia malengo yao.

“Kuna nafasi ya maboresho katika kila idara tunapoangalia katika klabu ya Manchester United. Tutaboresha kila mahali. Tunataka kuwa mahali Real Madrid walipo leo, lakini itatuchukua muda. Itahitahi madirisha 3 ya uhamisho ili kufikia malengo yetu,” alisema.