Kylian Mbappe uso kwa uso na godfather wake, CR7 kwenye robo fainali Euro2024

Hii huenda ikawa mara ya mwisho kwa Mbappe kupata nafasi ya kipekee ya kushiriki uwanja mmoja na godfather wake katika pambano la kimataifa, kwani Ronaldo anatarajiwa kustaafu kutoka soka la kimataifa miaka si mingi ijayo.

Muhtasari

• Ureno iliishinda Slovenia katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Euro 2024 kwenye Uwanja wa Frankfurt Arena huku Cristiano Ronaldo akitarajiwa kucheza toleo lake la mwisho la michuano hiyo.

Kylian Mbappe pamoja na Christiano Ronaldo
Image: KMbappe/X

Sasa ni rasmi kwamba Mfaransa Kylian Mbappe atakutana na ‘godfather’ wake katika malimwengu ya soka, Cristiano Ronaldo timu zao zitakapomenyana kwenye robo fainali ya kipute cha Euro 2024 mnamo Julai 6.

Ureno iliishinda Slovenia katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Euro 2024 kwenye Uwanja wa Frankfurt Arena huku Cristiano Ronaldo akitarajiwa kucheza toleo lake la mwisho la michuano hiyo.

Kwa upande mwingine, Ufaransa iliilaza Ubelgiji 1-0 katika pambano lake la hatua ya 16 bora huku Kylian Mbappe akiiongoza Ufaransa katika michuano mikubwa ya kimataifa kwa mara ya kwanza.

Ronaldo tayari ameshinda Euro na Ureno, lakini akiwa na umri wa miaka 39, anataka kuongeza kwenye mkusanyiko wake. Mbappe, kwa upande mwingine, anatazamia kuonja utukufu wa bara kwa mara ya kwanza.

Hii huenda ikawa mara ya mwisho kwa Mbappe kupata nafasi ya kipekee ya kushiriki uwanja mmoja na godfather wake katika pambano la kimataifa, kwani Ronaldo anatarajiwa kustaafu kutoka soka la kimataifa miaka si mingi ijayo.