Cucurella akiri kumshawishi Nico Williams kujiunga na Chelsea

Chelsea na Barcelona zimeonyesha ari ya kumsajili kinda huyo wa Uhispania

Muhtasari

•Marc Cucurella amekiri kuwa amejaribu kumshawishi Nico Williams kujiunga na Chelsea ila uamuzi wa mwisho ni kwake binafsi.

•Williams amekuwa nguzo kwa timu yake ya Athletic Club na Uhispania huku aking'ara kwenye mashindano ya Euro 2024.

Cucurella na Williams
Image: Facebook

Beki wa Chelsea, Marc Cucurella amekiri kuwa amekuwa akijaribu kumshawishi winga wa Athletic Club Nico Williams kuhamia Stamford Bridge msimu huu wa joto.

Wawili hao wote wanafurahia kampeni nzuri wakiwa na Uhispania kwenye Euro 2024, ambapo Williams anatarajiwa kupokea nia kubwa ya kuhama kutoka kwa vilabu kote Uropa.

 Cucurella alikiri winga huyo angekuwa usajili mzuri Camp Nou baada ya Barcelona kuonyesha ari ya kumsajili, ila alimsihi Williams kuhamia Chelsea badala yake.

"Ni mchezaji mzuri, anadhihirisha uwezo wake wote, ni jambo la kujivunia kuwa yuko kwenye timu yetu, kwamba ni mwenzetu na kwa wachezaji kama yeye kila kitu ni rahisi," Cucurella aliwaambia waandishi wa habari kule Uhispania.

"Angekuwa usajili mzuri kwa Barcelona, ​​lakini yote inategemea maoni yake. Ninamsukuma kusaini Chelsea. Mwishoni yote inategemea yeye. Yeye ni mdogo sana, na uzoefu mkubwa, na nadhani. atakuwa mchezaji mzuri."

Gazeti la AS ,hivi majuzi iliripoti kwamba Chelsea iko tayari kuanzisha kifungu cha kutolewa kwa Williams cha €58m (£49m), ingawa inasemekana kuwa 'The Blues' ni miongoni mwa pande zinazohusika na madai ya mshahara mkubwa wa winga huyo.

Williams amekuwa na mchango mkubwa kwa Uhispania, akianza michezo mitatu kati ya minne na kufunga bao muhimu katika ushindi wao wa hatua ya 16 bora dhidi ya Georgia kwenye kombe la Euro 2024.

Muda wake mzuri akiwa Athletic Bilbao, ambapo alifunga mabao manane na kutengeneza mabao 19 zaidi, na kuonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Euro kumemfanya kuwa tegemeo kubwa katika soko la usajili huku Barcelona na Chelsea wakiwa mbioni.