UEFA kuchunguza Demiral kufuatia ishara marufuku ya kusherehekea

Demiral alisherehekea bao lake la pili kwa ‘wolf salute’, ishara iliyo marufuku Ufaransa na Austria

Muhtasari

•Alisherehekea bao lake la pili kwa ‘wolf salute’, ishara inayohusishwa na kundi la itikadi kali za mrengo wa kulia la Gray Wolves ambalo linahusishwa na chama tawala cha Uturuki 

•"Ninajivunia sana kwa sababu mimi ni Mturuki, kwa hivyo baada ya bao nilihisi mshawasha sana na nilitaka kusherehekea hivyo, na nina furaha sana kuifanya." Alisema beki huyo.

Beki wa Uturuki Merih Demiral
Image: HISANI

Beki wa Uturuki Merih Demiral anachunguzwa na Uefa baada ya kuonekana kusherekea kwa utovu wa nidhamu kufuatia ushindi wa nchi yake dhidi ya Austria.

Demiral, 26, alifungia mara mbili Uturuki ambapo ilijikatia tiketi ya robo fainali ya Euro 2024 kumenyana na Uholanzi baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Austria.

Beki huyo wa Al-Ahli alisherehekea bao lake la pili kwa ‘wolf salute’, ishara inayohusishwa na kundi la itikadi kali za mrengo wa kulia la Gray Wolves ambalo linahusishwa na chama tawala cha Uturuki cha National Movement Party.

Demiral alisema salamu hiyo, ambayo imepigwa marufuku nchini Austria na Ufaransa, ilipangwa mapema iwapo angefunga.

"Nilikuwa na lengo kusheherehekea hivyo akilini baada ya kufunga," Demiral alisema.

"Ninajivunia sana kwa sababu mimi ni Mturuki, kwa hivyo baada ya bao nilihisi mshawasha sana na nilitaka kusherehekea hivyo, na nina furaha sana kuifanya." Alisema beki huyo.

Demiral alichapisha picha ya kusherehekea huko kwenye akaunti yake ya X na nukuu: "Ni furaha iliyoje yule anayesema mimi ni Mturuki!"

kwenye akaunti yake ya X na nukuu: "Ni furaha iliyoje yule anayesema mimi ni Mturuki!"

Uchunguzi wa Uefa umefunguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 31(4) kuhusiana na "tabia isiyofaa inayodaiwa" ya Demiral.

Iwapo atapatikana na hatia, Demiral anaweza kutozwa faini au kufungiwa asicheze huku Uturuki ikijiandaa kumenyana na Uholanzi katika robo fainali Jumamosi.

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham anachunguzwa kwa ishara aliyoifanya wakati wa ushindi wa hatua ya 16 bora dhidi ya Slovakia siku ya Jumapili.

Bellingham alionekana akifanya ishara ya kukaba kuelekea benchi ya Slovakia baada ya kufunga mkwaju wa juu katika dakika za lala salama.