logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eto'o atozwa faini ya Sh25.5m huku akiepuka malipo ya kupanga matokeo

Eto'o alikabiliwa na ukiukaji wa maadili, lakini ikapata ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji matokeo.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo06 July 2024 - 04:59

Muhtasari


  • •Eto'o alikabiliwa na ukiukaji wa maadili, lakini ikapata ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji matokeo.

Shirikisho la soka barani Afrika limemtoza faini ya $200,000 (Sh2.464m)   rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto'o, kwa ukiukaji wa maadili, lakini ikapata ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji matokeo.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilianzisha uchunguzi kuhusu mwenendo wa Eto'o mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupokea "taarifa zilizoandikwa kutoka kwa wadau kadhaa wa soka wa Cameroon".

Jopo la nidhamu lilibaini kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne "amekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni za maadili, uadilifu na uanamichezo" za Caf kwa kutia saini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya kamari ya 1XBET.

Mawakili wa Eto'o wamesema watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved