Southgate awataka wachezaji wake kuweka historia kwenye mechi dhidi ya Uholanzi

Muhtasari

•Southgate amewataka wachezaji wake kuonyesha ubora kwenye mechi dhidi ya Uholanzi ili kuwaacha mashabiki na kumbukumbu za kutosha.

•Mshindi kati ya Uingereza na Uholanzi atachuana na  Uhispania kwenye fainali ya Euro 2024 Julai 14,2024.

Kocha wa Uingereza
Gareth Southgate Kocha wa Uingereza
Image: BBC

Kocha  wa  Uingereza,Gareth Southgate amewataka wachezaji wake kuweka usiku wa kukumbukwa  watakapochuana na Uholanzi kwenye nusu fainali ya Euro 2024.

Kikosi cha Southgate kitakuwa timu ya kwanza ya Uingereza kutinga fainali ya mashindano makubwa nje ya nchi ikiwa watapata ushindi dhidi ya Uholanzi katika uwanja wa Westfalenstadion, Dortmund.

Southgate alitupiwa vikombe vya bia vya plastiki na mashabiki katika hatua ya makundi, sasa ana nafasi ya kuiongoza England kutwaa taji kubwa tangu 1966 huku akikabiliwa na kibarua hii leo kwenye nusu fainali.

"Ninaweza kukumbuka jinsi ilivyokuwa kutoka kwa mashindano yaliyopita, kwa hivyo ni moja ya bahati ya kuiwakilisha Uingereza ambayo una nafasi ya kuwapa watu kumbukumbu ambazo hukaa nao kwa muda mrefu," Southgate alisema.

Kocha huyo anatarajiwa kufanya mabadiliko kwa kikosi chake cha kwanza, hasa baada ya beki  Marc Guehi  kurejea.

Southgate ameiongoza timu yake katika hatua ya nusu fainali ya michuano yake mitatu kati ya minne mikuu na anasema ametumia uzoefu wake katika mechi nne za mwisho katika maandalizi yake ya kukabiliana na kikosi cha Ronald Koeman.

England ilikuwa haijatinga nusu fainali ya michuano mikubwa tangu mwaka 1996 kabla ya Southgate kuwasili lakini baada ya kutinga hatua ya nne ya fainali za kombe la dunia 2018 ukakamvu zaidi umechipuka.

Mshindi kati ya Uingereza na Uholanzi atachuana na Uhispania iliyojikatia tiketi baada ya kuwabwaga Ufaransa  2-1 .

Fainali ya Euro 2024 itachezwa  Jumapili ,Julai 14,2024.