logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Euro & Copa America: Uhispania, Argentina zashinda fainali za mashindano ya bara

Argentina ilishinda 1-0 katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika bila bao.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo15 July 2024 - 04:40

Muhtasari


  • •Fainali za shindano kubwa zaidi barani Ulaya, Euro, na michuano mikubwa kabisa ya Amerika, Copa America, zilichezwa katika nyakati tofauti.
  • •Argentina ilishinda 1-0 katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika bila bao.

Usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu ulikuwa na matukio mawili makubwa ya soka.

Fainali za shindano kubwa zaidi barani Ulaya, Euro, na michuano mikubwa kabisa ya Amerika, Copa America, zilichezwa katika nyakati tofauti.

Uhispania ilishinda taji la Euro 2024 kwa kuifunga England katika fainali zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi zilizochezwa kwenye uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin, Ujerumani.

Mechi hiyo iliyochezwa saa nne usiku wa Jumapili ilimalizika kwa mabao 2-1 huku Uhispania ikinyakua ushindi huo dakika ya 86 kupitia kwa kiungo Mikel Oyarzabal.

England walikuwa wamerejea kwenye mechi baada ya kiungo wa Chelsea Cole Palmer kuingia uwanjani na kufunga bao la kusawazisha dakika ya 73.

 Bao hilo lilikuwa limefuta bao la Nico Williams alilofunga katika dakika ya 47, lakini halikutosha kuzuia England kushindwa.

Katika fainali ya pili iliyochezwa mwendo wa saa kumi asubuhi, Argentina ilishinda 1-0 katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika bila bao.

Mshambulizi wa Inter Milan Lautaro Martinez alifunga bao pekee katika mechi hiyo dakika za lala salama baada ya timu zote mbili kufanya majaribio kadhaa ya kufunga.

Mechi hiyo ilijawa na mvutano mkubwa huku Argentina na Colombia zikifanya majaribio mengi ya kufunga.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved