Fainali ya mashindano ya Copa America kati ya Argentina na Colombia ilicheleweshwa kwa zaidi ya saa moja usiku wa kuamkia Jumatatu.
Hii ilikuwa baada ya maelfu ya mashabiki wasio na tikiti kuvurutana na walinzi na kujaribu kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Hard Rock, mji wa Miami Gardens, jimbo Florida.
Mechi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuanza saa tisa asubuhi ya Jumatatu lakini iliishia kuanza saa kumi na dakika 15 asubuhi.
Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha walinzi wakizozana na mashabiki walipokuwa wakikimbia kwenye kiingilio na kujaribu kuvunja milango ya uwanja.
Polisi walifanikiwa kufunga milango, na kusababisha watu wengi kukwama nje ya uwanjza wakijaribu kuingia kabla ya mechi kuanza.
Timu zote mbili zilitolewa nje ya uwanja huku fujo zikiendelea nje.
Shirikisho la kandanda la Amerika Kusini CONMEBOL lilipeleka mbele muda wa kuanza mara tatu kutoka saa tisa asubuhi hadi 3:30 asubuhi, hadi 3:45 asubuhi na hatimaye 4:15 asubuhi, wakati ambapo hatimaye timu ziliweza kujipanga uwanjani kwa wimbo wa taifa. na kuanza mechi.
"Kwa kutarajia fainali ya Copa America usiku wa kuamkia leo, maelfu ya mashabiki bila tiketi walijaribu kuingia kwa nguvu uwanjani, hivyo kuwaweka mashabiki wengine, maafisa wa usalama na wasimamizi wa sheria katika hatari kubwa.
Walinzi wamefunga milango ili kudhibiti mchakato wa kuingia kwa polepole zaidi. hakikisha kuwa kila mtu yuko salama," taarifa kutoka kwa msemaji wa Uwanja wa Hard Rock ilisema.
Polisi wa mji wa Miami-Dade walisema kulikuwa na matukio kadhaa kabla ya milango kufunguliwa kwenye uwanja huo.
"Matukio haya yametokana na tabia mbaya ya mashabiki kujaribu kuingia uwanjani,” walisema kwenye mitandao ya kijamii.